• Amekiri anatafuta mwanaume wa kuchumbiana naye mwaka huu 2022
• Alieleza kuwa haoni kama kuna mwanamume aliyechumbiana naye mwaka jana atakaemchumbia mwaka huu.
• Isitoshe aliwatania wapenzi wake wa zamani kwa kuwambia waende kuchukua vyeti vyao kwani vishatoka.
Sosholaiti Amber Ray amekiri anatafuta mwanamume wa kuchumbiana naye mwaka huu 2022.
Kupitia ukurusa wake wa instagram, alieleza kuwa haoni kama kuna mwanamume aliyechumbiana naye mwaka jana atakuwa naye mwaka huu.
Mama huyo wa mtoto mmoja aliwataarifu wanaume wapya wanaomtamani na wako tayari kumchumbia waanze kutuma maombi yao haraka iwezekanavyo kabla nafasi kufungwa.
Isitoshe aliwatania wapenzi wake wa zamani kwa kuwambia waende kuchukua vyeti vyao kwani viko tayari.
"Wale niliotoka nao mwaka 2021 vyeti vyao vimetoka, tafadhali njoo uchukue na 2022 uandikishaji wa wapenzi wapya unaendelea, ingawa nafasi ziko finye."
Amber Ray alifunga ndoa na mmiliki wa Matatu, Jimal Rohosafi lakini ikadaiwa wapenzi hao waliachana kwa madai kwamba mume wake alikuwa na mpango wa kando.