Julia Fox akiri ni mpenzi wa sasa wa Kanye West

Muhtasari

•Julia alieleza kwamba atamani pesa za mwimbaji ila mapenzi anayompa yanamtosha na kukiri kama ni pesa amewai kuwa kwenye mahusiano na watu walio na pesa kumliko Kanye West

• Kanye West ambaye walikosana na Mama wa watoto wake Kim Kardashian.siku ya sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bintiye Chikago.

Kardashian alimficha Baba wa mtoto eneo ambalo sherehe hizo zilikuwa zimeandaliwa lakini rafiki yake alimjulisha walikokuwa.

julia fox
julia fox
Image: hisani

Mwigizaji Julia Fox amejitokeza na kueleza bayana kuhusu mahusiano yao baina yake na Kanye West huku akikiri anampenda rapa huyo.

Hivi majuzi kumekuwa na habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba Julie anatamani pesa za Kanye West na hana mapenzi kwake.

Kutokana na kauli hio, Julie alisema kwamba hatamani pesa za mwanamuziki huyo ila mapenzi anayompa yanamtosha na kukiri kama ni pesa amewai kuwa kwenye mahusiano na watu walio na pesa kumliko Kanye West.

“Watu wamekuwa wakisema mimi niko na Kanye West kwa kuwa nataka kutengeneza pesa kwa sababu yeye ni milionaire. Wakati mwingine watu wanasema ni mbinu yangu ya kutengenza kiki lakini siko hivo kama ni pesa nimekaa na watu wenya pesa kumshinda Kanye,” alisema Julia Fox.

Kanye West ambaye walikosana na Mama wa watoto wake Kim Kardashian siku ya sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bintiye Chicago.

Kardashian alimficha Baba wa mtoto eneo ambalo sherehe hizo zilikuwa zimeandaliwa lakini rafiki yake alimjulisha walikokuwa.

Kutokana  na ukaribu wa Kanye west na Julia Fox wanamitandao wamekuwa wakisema ni njia ya kufanya Kim kusikia vibaya.