'Mnazuia baraka zangu' Willy Pozee awambia wanaomuita Mkunaji

Muhtasari

• Alipakia video akiwaeleza  mashabiki wake kwamba mwaka huu mpya anawaomba waache kumwita jina hilo

• Sitaki kuitwa bwana mkunaji kwa sababu mnazuia baraka za wimbo mpya wa  toto kutambulika

 

Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Msanii Wilson Abubakar Radido almaarufu Willy Pozee amelezea kukerwa na wanamitandao wanaomuita Bwana  Mkunaji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha video akiwaeleza  mashabiki wake kwamba mwaka huu mpya anawaomba waache kumwita jina hilo.

"Tafadhali, watu wangu, acheni kuniita bwana mkunaji. sitaki kuitwa bwana mkunaji kwa sababu mnazuia baraka za wimbo mpya  wa  toto kutambulika," Willy alieleza.

Hivi majuzi Willy Paul alitoa taarifa akieleza maana fiche ya mkunaji.

,'Mkunaji' ni jina ambalo linahusishwa na mambo mabaya na kudai matatizo mengi  yamekuwa yakimkumba kutokana na jina hilo.

"Ninapenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wote kuwa kuanzia leo sitakuwa natumia jina la 'MKUNAJI', ni baya na sitaki kujihusha nalo! Tangu nilipokubali jina hilo nimekuwa na matatizo mengi sana"alisema Pozee.

Kulingana naye wimbo ambao ametoa mwaka huu haufanyi vizuri kwa sababu ya itikadi za jina ambalo mashabiki wake walimbandika.