Msanii Eko Dydda kuwania kiti cha MCA Mathare kaskazini

Muhtasari
  • Msanii Eko Dydda kuwania kiti cha MCA Mathare kaskazini
Eko Dydda
Image: INSTAGRAM

Msanii na rappa maarufu Emmanuel Dydda almaarufu Eko Dydda, ametangaza kuwania kiti cha MCA Mathare Kskazini.

Katika siku za hivi majuzi tumewaona na kushuhudia wasanii na watangazaji mbali mbali wakijiunga na ulingo wa siasa kuwania viti tofauti katika uchaguzi mkuu wa Agosti.

Dydda alieleza kuwa alichagua kukabiliana na changamoto hiyo baada ya kuwa raia asiyeridhika kwa muda mrefu.

Akipendekeza kuwa viongozi waliochaguliwa wameendelea kukatisha tamaa taifa, mwimbaji huyo wa Niko Na Reason alisisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu ni fursa kwa sera kujirekebisha.

Mwimbaji huyo hakutaja ikiwa atajiunga na chama cha kisiasa kabla ya uchaguzi.

Tangazo hilo lilipongezwa na wasanii wenzao Holy Dave na Kriss Erroh ambao waliahidi kumuunga mkono mwenzao.

"Tumesema wabadilishe na maybe hawaoni kitu ya kubadilisha, so itabaki tujibadilishie inchi wenyewe, chukua kura sasa tubadilishe hizi mtaa KIMANGOTOS KIMANGOTOS hatulegezi kamba. MIK CULTURE love culture everywhere," Alisema Eko Dydda.