Eric Omondi afichua mbona anatamani kupata watoto wa kike pekee sio wa kiume

Muhtasari

•Mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama amesema baada ya kupata mchumba anakusudia kupata watoto wawili wa kike naye.

•Omondi anaaminika kuwa na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba na mtangazaji Jacque Maribe.

Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi amesisitiza kuwa anakusudia kupata jiko na kuazisha familia hivi karibuni

Omondi ambaye mwaka huu atakuwa anafikisha miaka 40 mwezi ujao amekiri kuwa umri wake umemshinikiza kuanza mpango wa ndoa.

Mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama amesema baada ya kupata mchumba anakusudia kupata watoto wawili wa kike naye.

"Nafikisha miaka 40 mnamo Machi 9. Hapa kwangu hakuna mke wala watoto. Nawahitaji mwaka huu. Nataka watoto wawili wa kike" Omondi alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Omondi alieleza kuwa anatamani sana kupata watoto wa kike kwa kuwa alizaliwa na kulelewa katika mazingira iliyo na wanaume wengi.

Alifichua kuwa ana kaka wengi na dada mmoja tu huku akisema angependa kuleta utofauti katika familia anayokusudia kuanzisha.

"Katika familia yetu kuna msichana mmoja tu, dadangu Irene Omondi. Niko na mtu lakini sina bibi. Nataka niwe na familia" Alisema.

Mchekeshaji huyo anaaminika kuwa na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba na mtangazaji Jacque Maribe.