Kipusa atoka Dubai akitaka kupachikwa mimba na Harmonize

Muhtasari

• Kidosho mmoja amewasili Tanzania  kutoka Dubai kutafuta mwanamuziki nguli wa bongo Fleva  Harmonize.

• Kipusa huyo anasema amekuwa akivutiwa sana  na mwonekano wa Harmonize, mwonekano ambao umekuwa ni kama sumaku iiliyokuwa ikimvuta kwake.

 

Harmonize
Harmonize

Kidosho mmoja amewasili nchini Tanzania  kutoka Dubai kutafuta mwanamuziki nguli wa bongo fleva  Harmonize.

Kipusa huyo alisema kwamba amekuwa akivutiwa sana  na mwonekano wa Harmonize, mwonekano ambao umekuwa ni kama sumaku iliyokuwa ikimvuta.

Alieleza amekuwa na ndoto ya kuzaa na mwanamuziki huyo, ndoto ambayo imemlazimu kuachana na mpenzi wake na  kuzuru Tanzania kutafuta mwanamuziki huyo angalau amweleze sababu zake.

Kupitia video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii  mrembo huyo amekiri kutamani kuwa na mwanamuziki huyo, na kueleza kuwa yeye hatafuti kiki ila anachotaka  ni kupata ujauzito wa msanii huyo.

Kama ilivyoada mwamba ngoma huvutia pande yake alieleza kuwa ashawaeleza wazazi wake sababu zake za kuzuru nchi ya Tanzania na wote wamekubaliana naye.

"Nahitaji  kupata ujauzito na Harmonize, nataka niwe na damu yake, kutokana na ninavyo mkubali na kumpenda.   Hicho ndicho kimenitoa Dubai kuja hapa, sitaki kiki sitaki pesa, pesa ninazo najua kutafuta pia,  kwa hivyo ninachotaka nikutane naye,” alisema mwadada huyo.

Aliendelea kusema,”...mimi nina mpenzi wangu, kwa sasa yuko Dubai,  kulingana na jinsi nilivyomzoea Harmonize wakati  mwingine namtaja, kuna kipindi nikiwa na mpenzi wangu  badala ya kumtaja yeye nikamtaja tu Harmonize,” alisema

Kauli ya kipusa huyo imejiri wakati Harmonize amepewa mapenzi motomoto na kidosho mzungu  anayetambulika kama Briana.