Kupata Mpenzi ilikuwa ngumu-Muigizaji wa Tahidi High asimulia

Muhtasari

•Muigizaji wa Zamani wa Tahidi High Dennis Mugo almaarufu OJ ameeleza changamoto alizokumbana nazo wakati alikuwa akitafuta mchumba.

Dennis Mugo almaarufu OJ
Dennis Mugo almaarufu OJ
Image: HISANI

Muigizaji wa Zamani wa Tahidi High Dennis Mugo almaarufu OJ ameeleza changamoto alizokumbana nazo wakati alikuwa akitafuta mchumba.

Muigizaji  huyo  alieleza kuwa  jukumu alilokuwa amepewa kuigiza kwenye kipindi hicho lilimfanya aonekane kama yeye ni mwanamume ambaye hawezi kuwa mwaminifu kwenye ndoa.

Akihojiwa na Mungai Eve, OJ alisema watu huanaamini wanachokiona na hata ukijaribu vipi kujitetea itakuwa ngumu kuaminika.

“Watu wanakuhukumu kwa kile wanachoona unafanya kwenye show, inachosha wakati mwingine. Hata kwenye uhusiano iliniathiri, nilikuwa single kwa mwaka mmoja kwa sababu wasichana walidhani mimi ni playboy na nina wasichana wengi. Ilikuwa ngumu. hata kumshawishi mama mtoto wangu wa sasa," alisema OJ.

Aliongeza kuwa watu wengi  ambao wamekuwa wanafuatilia kupindi hicho walikuwa wanamhukumu kutokana na maudhui aliyokuwa akikuza kwenye kipindi hicho ambacho kilibukia  kuwa bora miongoni mwa watazamaji.

"Siku moja, nilikuwa na Miss Morgan tumeketi katika hoteli na mtu alipita karibu na alikuwa na hasira kwamba alikuwa na mwanafunzi wake katika mgahawa. Mwanamume huyo hata aliketi karibu nasi na alianza kutufundisha kuhusu hilo akisema sisi ni mifano mbaya."