Thee Pluto atoa sababu za kutoishi na mchumba wake

Muhtasari

• Mwanablogu Thee Pluto hatimaye ametoa sababu ya kutoishi na mchumba wake Felicity katika nyumba moja.

• “Mimi natoka jamii ya wakikuyu na sisi tunaamini  sana katika tamaduni, kwa hivyo lazima nizifuate,” Thee Pluto alisema.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Thee Pluto

Mwanablogu Thee Pluto hatimaye ametoa sababu ya kutoishi na mchumba wake Felicity katika nyumba moja.

Akizungumza na wanahabari, Pluto alisema kwamba yeye  anakumbatia sana mila na tamaduni za jamii ya Agikuyu na kulingana na sheria zilizopo ni kwamba huwezi kuishi na mchumba wako katika nyumba moja iwapo hujalipa mahali na kukamilisha shughuli zote za kifamilia.

“Mimi natoka jamii ya wakikuyu na sisi tunaamini sana katika tamaduni, kwa hivyo lazima nizifuate,” Thee Pluto alisema.

Aidha, aliongezea kwamba baada ya kukamilisha mikakati yote basi ataanza kuishi na mpenzi wake kwenye nyumba moja kama mume na mke.

Thee Pluto alilazimika kujibu swali hilo kutokana na madai kwamba huenda tena wameachana na mchumba wake baada ya kurudiana wiki chache zilizopita.

Ifahamike kwamba ni juzi tu ambapo mwanablogu huyo amenunua nyumba mpya katika mtaa wa Lavington huku wengi wa mashabiki wake wakimkshifu kwa kile walichokisema kuwa Pluto anatumia na kuharibu pesa nyingi kulipa kodi ya nyumba.

Ila kwa upande wake, alijitetea na kusema kwamba alihamia sehemu hiyo kwa kuwa ipo karibu na mjini ambapo anafanikisha shughuli zake nyingi za kibiashara.