Sipo kwenye mahusiano na Thee Pluto - Wangui Nganga

Muhtasari

• Mgombea wa kiti cha mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Nairobi, Wangui Nganga amekana madai ya kuwa kwenye mahusiano na mzalishaji video katika mtandao wa YouTube, Thee Pluto.

• Akizungumza na moja ya wanahabari nchini, kiongozi huyo amesema kwamba yeye na Pluto ni rafiki wa karibu tu na wala hawajahi kuwa katika hali ya kimapenzi.

• Aidha amewarai wakaazi wote kujisajili kama wapigakura ili kuwawezesha kuwachagua viongozi wanaowapenda na ambao watashughulikia masilahi yao

Instagram KWA HISANI
Instagram KWA HISANI
Image: Thee Pluto

Mgombea kiti cha mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Nairobi, Wangui Nganga amekana madai ya kuwa kwenye mahusiano na mzalishaji video katika mtandao wa YouTube, Thee Pluto.

Akizungumza na moja ya wanahabari nchini, kiongozi huyo amesema kwamba yeye na Pluto ni rafiki wa karibu tu na wala hawajahi kuwa katika hali ya kimapenzi. Amesisitiza kuwa, ni watu tu ambao wanataka kuharibu jina lake kwa umma.

Kuhusu kumnunulia Thee Pluto gari,        Nganga amekana madai hayo pia na kusema kwamba alihudhuria hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake Pluto ili kukutana na vijana wengine ambao wanajituma katika kazi zao mbalimbali na ni vipi wanaweza kushirikiana katika mchakato wa kuboresha hali zao za kikazi na kimaisha kwa ujumla.

Huku akiwa anawania wadhifa ambao una upinzani mkali, Wangoi Nganga amesema kwamba anafanya mazungumzo na viongozi mbalimbali ili kufahamu matatizo wanayokumbana nayo katika shughuli zao za kikazi ali ajifunze na kutafuta mbinu mbadala za kufanikisha ajenda zake katika kaunti ya Nairobi.

Aidha amewarai wakaazi wote kujisajili kama wapigakura ili kuwawezesha kuwachagua viongozi wanaowapenda na ambao watashughulikia masilahi yao.Hii ikiwa mara ya pili kiongozi huyo anawania wadhifa wa mwakilishi wa wanawake, amesema kwamba amejifunza mambo mengi na anaamini kwamba atawahi cheo hichi katika uchaguzi mkuu unaoratibiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.