Singetaka mume wangu aoe mke wa pili - Zamaradi

Muhtasari

• Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Zamaradi amesema wazi kwamba hangetaka mume wake aoe mke wa pili.

• “Sijui mbona watu wanachukulia jambo hilo poa tu, sio rahisi wanavyofikiria,” Zamaradi alisema.

Instagram KWA HISANI
Instagram KWA HISANI
Image: Zamaradi

Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Zamaradi amesema wazi kwamba hangependa mume wake aoe mke wa pili.

Akizungumza katika mahojiano na Millard Ayo, Zamaradi alisema kwamba yeye ni mtu mwenye wivu katika mapenzi na kwamba hangependa kuwepo na mke mwenza.

Aidha alikiri kwamba kuoa mke wa pili sio jambo rahisi na kwamba kunapaswa kuwepo majadiliano ya kina kati ya wanandoa ili kuhakikisha kila mmoja anaridhia uamuzi huo.

“Sijui mbona watu wanachukulia jambo hilo poa tu, sio rahisi wanavyofikiria,” Zamaradi alisema.

Zamaradi pia alizungumzia kuhusu jinsi yeye na mchumba wake wanavyotatua changamoto zao akisema wanahakikisha kadri  ya uwezo wao kwamba kuna amani wakati wote katika ndoa yao.

Akigusia suala la kumtundika mumewe kwenye bango, mtangazaji huyo alisema kwamba alifanya hivo ili dunia ipate kuelewa ni kwa jinsi gani anampenda numewe na kwamba yuko tayari kulipigania penzi lao kwa hali na mali.