Eric Donaldson kutumbuiza Kenya kwenye Ziara ya Amani

Muhtasari

•Mwanamuzi kutoka Jamaica Eric Donaldson ametangaza kuzuru nchi ya Kenya kutumbuiza wapenzi wa muziki wa Reggae.

Mwanamuziki wa Jamaika Eric Donaldson
Mwanamuziki wa Jamaika Eric Donaldson

Mwanamuzi kutoka Jamaica Eric Donaldson ametangaza kuzuru nchi ya Kenya kutumbuiza wapenzi wa muziki wa Reggae.

Donaldson  ni maarufu kwa wimbo wa ‘Cherry Oh Baby’ anatazamiwa kuzuru nchini mnamo Julai 5 hadi Julai 30 mwaka huu ambapo atatumbuiza miji kadhaa nchini.

Ziara hiyo itakuwa ya miezi miwili ambapo atazuru miji ya Eldoret, Nakuru, Meru, Mombasa akijumuisha wasanii wa humu nchini.

 Ziara hiyo imeandaliwa na ‘Umoja Splash Festival na kusimamiwa na Ngoma Tucheze ambao wanasifika kwa kuleta wasanii wakubwa wa reggae nchini. 

Kulingana na wandalizi lengo la tamasha hilo ni kuhubiri amani kote nchini wakati ambao uchaguzi unakaribia.

 "Kupitia ziara hii, tunanuia kuhubiri na kuendeleza amani kabla ya uchaguzi na vile vile kuwapa Wakenya tafrija isiyoweza kusahaulika na pia kuwatia moyo wa umoja na kuwa Wakenya,” Wandalizi hao walibainisha.