Wakenya wengi hufanya 'streaming' ya muziki kupitia Boomplay

Muhtasari

• Jukwaa la kusikiliza miziki kwa njia ya mtandao la Boomplay limetajwa kuwa pendwa na Wakenya wengi kulingana na Music Chart 254.

Boomplay Kenya
Image: Facebook

Jukwaa la kupakua miziki la Boomplay liliongozwa wiki iliyopita kama jukwaa ambalo ni pendwa zaidi na Wakenya wengi katika kupakua miziki kwa njia ya ‘streaming’.

Kulingana na utafiti wa Music Chart 254, Boomplay ilitumika sana wiki iliyopita na Wakenya wengi kuskiza miziki na albamu mbalimbali za Kenya kwa njia ya mtandao huku ikifuatiwa na jukwaa lac Deezer.

Jukwaa la Boomplay lilishuhudia streams 44 za ngoma singles na streams za albamu 31 huku jukwaa hilo likifuatwa na lile la Deezer ambapo streams za singles zilikuwa 29 na albamu zikiwa 30.

Jukwaa la Apple Music lilishikilia nafasi ya tatu kwa wiki iliyopita ambapo ngoma singles 24 zilisikilizwa kwa njia ya mtandao huku albamu 29 zikiwa zimefuatiliwa kupitia kwa jukwaa hilo.

Mitandao na majukwaa mengine ambayo pia Wakenya walitumia kupata miziki kwa njia ya kimtandao au ukipenda ‘streaming’ ni Mdundo, Audiomack na YouTube.

Jambo lingine ambalo pia hatuwezi tamatisha bila kuligusia almradi limejitokeza ni kukosekana kwa jukwaa la Spotify katika majukwaa pendwa ambayo Wakenya walitumia kufuatilia miziki wiki iliyopita.

Ikumbukwe jukwaa la Spotify ni jukwaa pendwa zaidi haswa katika bara la Uropa na humu nchini limefika miaka michache ijayo ambayo wamejaribu sana kujitangaza na kupata nafasi yao katika nyoyo za wapenda muziki nchini lakini ni kama bado ipo kazi kubwa ya kufanywa na afisa masoko wa jukwaa hilo.

Music Chart 254
Image: Instagram