Jalang'o kuachia Jalang'o TV, atangaza nafasi za kazi

Muhtasari

• Jalang'o atangaza rasmi kuacha kujihusisha na Jalang'o TV na kutangaza nafasi mbalimbali za kazi kwa wenye uwezo na vigezo tajika.

Jalango
Jalango
Image: Hisani

Mchekeshaji na mwanasiasa Jalang’o ametangaza kuondoka rasmi kwenye mambo ya utqangazaji na kusema kwamba anatafuta watangazaji na wanahabari ili awaajiri katika runinga yake ya mtandoni Jalang’o TV.

Mwanasiasa huyo ambaye analenga kuwania ubunge wa Lang’ata kwa tikketi ya chama cha ODM ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema kwamba anataka watu katika vitengo mbalimbali ili kuwapa kazi hiyo ambayo haoni akiendelea kuifanya kwa sababu anataka kuingia zaidi katika siasa.

“Si siri tena kwamba niko katika siasa na hili halitaniruhusu niendelee kukaa katika Jalang’o TV mara nyingi kama awali. Kwa hiyo bado tunaendelea kutafuta wakuza maudhui wakubwa ili kuchukua nafasi tatu za wahariri, tatu za watangazaji wa zamu, tatu za wanakamera na moja ya mbunifu wa picha,” aliandika Jalang’o.

Image: INSTAGRAM

Amewataka wafuasi na mashabiki wa Jalang’o TV kuwa na Subira kwani hivi karibuni atatoa muelekeo wa jinsi ya kutuma maombi ya kazi hizo kwa wale wanaozitaka.

Jamaa iko kazi!