Diamond na Zuchu ni 'couple' ya nguvu, adai Mange Kimambi

Muhtasari

• Mwanaharakati Mange Kimambi amefunguka kwamba mapenzi ya Diamond na Zuchu yana uwuiano mzuri sana mpaka yanamfanya aone gere.

Instagram
Diamond na ZXuchu wakati wa uzinduzi wa EP ya FOA Instagram
Image: Mange Kimambi

Mwanaharakati mwanamke mwenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania Mange Kimambi hatimaye amewataja Diamond na Zuchu kuwa wanadoa wa nguvu sana ambao anawalilia ngoa na kuwafagilia kwa kiasi kikubwa.

Kimambi aliandika kwenye ukurasa wake wa instagram akiwasifia wawili hao kwa jinsi walivyokaribiana jukwaani kimahaba wakati wa uzinduzi na kusikilizwa kwa EP ya Diamond Paltnumz ya FOA usiku wa kuamkia Ijumaa.

Kimambi amewamiminia wawili hao makopakopa na kusema kwamba ndio wanandoa wake pendwa sana kwa sasa na anawakubali mpaka anazimia.

Mange Kimambi anazidi kuandika katika post ndefu akisema kwamba amemjua Diamond kwa muda mrefu lakini hawajahi ona akiwa na mwanamke mwenye wanaendana naye kama Zuchu.

Haki this is my favorite couple in the whole world right now. Hata Ciara na mume wake nyuma…Toka nimemjua Dai Zuchu ndo mwanamke wa kwanza nimemuona na Dai na nikaikubali couple. I will tell you why? I think for the first time since Wema Sepetu Diamond is actually in love. Kaacha woote wale kaangua hapa? Aisee ni kwamba moyo umemzidi nguvu maana kama ni kiki angeipata kwa Misa au kwa Bi Tuks kiki zaidi ya hii. Hapa kapenda tu!!!” aliandika Kimambi

Pia mwanaharakati huyo ambaye ameolewa na mzungu anazidi kuandika kwa kuonesha kusikitishwa kwake na wale wanaosema kwamba Diamond na Zuchu hawaendani na kusema kwamba wengi wanaosema hivyo ni wale wanaomuonea gere na pengine wanataka awe na makalio yaliyofanyiwa upasuaji kwa kuongezwa nchini Uturuki kama ambavyo wanawake wengi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakifanya kisiri.

 “Sijui why watu wanasema hawaendani bwana mi nawapenda mpaka naumwa. Eti Zuchu sio mzuri, nyie Zuchu ni mzuriii, tatizo mnataka na yeye awe na matako yenu ya uturuki. Zuchu is super cute. Alafu mkae mkijua wanaume hawaoi eti sababu tu demu mzuri, mademu wazuri wapo kibaoooo na wamedoda mpaka wanalea wana, msinifanye nikawataja saa hizi. Maishani usililiee uzuri lilia bahati,” alishauri Kimambi.

Kimambi ambaye vkwa muda mrefu amekuwa akitofautiana na wengi kuhusu Diamond anasisitiza kwamba hata kama hatimaye ameikubali ‘couple’ hiyo lakini bado yeye msimamo wake ni pale pale kwamba ako kwa Alikiba ambaye ni mbaya wake Diamond kimuziki.

“Haki sikudhani kuna siku ntaja kuipenda couple ya Dai na mtu yoyote yule ila Zuchu kanibadilisha haki…. Isingekuwa nimelogwa na yule mtoto wa kariakooo haki ningekuwa chawa wao jinsi nimeipenda hii couple. Ila sasa mi team KIBA so vichambo vitabaki pale pale. Yani wakiangaliana tu mie hoi,yani wana chemistry moja kaliiiiii…” alitamatisha Mange Kimambi.