Babalevo asutwa kwa kuvalia chupi yenye nembo feki

Muhtasari

• Msanii Babalevo ameshambuliwa na mashabiki kwa kile walichokisema kuwa alikuwa amevalia chupi ghushi.

• “Mpaka sasa sijaona ubaya wowote, nachojua chupi ni chupi tu,” Babalevo aliandika.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Babalevo

Msanii Babalevo ameshambuliwa na mashabiki kwa kile walichokisema kuwa alikuwa amevalia chupi ghushi.

Kupitia picha aliyoipakia kwenye mtandao wa Instagram, Babalevo alionekana kuvalia chupi yenye nembo ya ‘Calvin Kelin’ badala ya nembo halisi ya ‘Calvin Klein.’

Babalevo alichapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram akisema kwamba haoni tatizo lolote kwani chupi ni chupi tu, maadamu inatekeleza wajibu wake wa kufunika uchi.

“Mpaka sasa sijaona ubaya wowote, nachojua chupi ni chupi tu,” Babalevo aliandika.

Baadhi ya wasanii pia kama vile Ommy Dimpoz walichangia mjadala huo huku akiandika kimzaha tu kwamba “…nashangaa watu wana wivu sana, kwani Calvin Kelin amezua?”

Kuna asilimia ya mashabiki waliosimama upande wake huku wengine wakimtaka kuvalia mavazi yenye nembo halisi kwa kuwa  yeye ni msanii mkubwa.

Mara kwa mara watu maarufu wamejikuta katika hali tata na mashabiki wao kutokana na mavazi yao, huku washikadau mbalimbali wakiwataka mashabiki kufahamu kwamba wasanii hao bado ni binadamu  tu.