Nitamuoa mke wako! meneja wa mbogi genje amuambia KRG

Muhtasari

• Meneja wa kundi la Mbogi Genje Elvis Makutsa amemchoma mkuki mkali kwenye kifua KRG the Don baada ya kumuambia atamuoa aliyekuwa mke wake.

• Hii ni kutokana na msururu wa ugomvi baina na KRG na kundi hilo la gengetone kutokana na kile kilitajwa kwamba the Don aliwatapeli hela.

Meneja wa Mbogi Genje Elvis Makutsa na Rappa KRG the Don
Meneja wa Mbogi Genje Elvis Makutsa na Rappa KRG the Don
Image: Instagram

Ugomvi kati ya msanii wa dancehall KRG the Don na kundi la gengetone la Mbogi Genje umeonekana kuchukua mkondo tofauti kabisa ambao wengi hawakuwa wameutarajia baada ya meneja wa vijana hao kujitosa ulingoni kumenyana na KRG moja kwa moja sasa.

Ugomvi ulianza baada ya kundi hilo la gengetone la Mbogi Genje kumtuhumu KRG kwa kuwatapeli pesa alizotakikana kuwakabidhi ambapo KRG alijitokeza wazi na kujibu madai hayo kwa kuwaita vijana hao kuwa ni maskini.

Baadae the Don alikataa katakata kwamba hana neno lolote la kuomba msamaha kwa kile alichokitamka juu ya Mbogi Genje.

Hivi majuzi mejena wa kundi hilo Elvis Makutsa alionekana akijivinjari na aliyekuwa mke wa KRG katika sehemu moja ya kujiburudisha.

Hili lilizua maneno mengi mitandaoni huku wengi wakitaka kujua KRG anahisi aje akiona aliyekuwa mke wake ambaye bado kesi ya kutalikiana iko mahakamani, KRG alipuuzilia mbali na kusema kwamba yeye hamjui na anashughulika kulea watoto wake ambao alisema wazi eti hawana mama.

Makutsa kwa kumjibu aliandika kwenye instastories zake akimchimba mkwara mzito KRG kwa kumuambia kwamba yeye si Don kama anavyojiita bali ni Con, kwa maana ya tapeli.

“Unadai kwamba wewe ni Don (con) lakini nitamuoa mke wako #amini,” aliandika Makutsa.

Wengi sasa wanangoja KRG kutoa tamko lake kwa meneja Makutsa.

Chukua njugu zako uketi mkao wa kula maana huu ugomvi unaelekea kilele chenyewe sasa.