"Nyinyi mko chini sana hamniwezi," KRG awasuta Mbogigenje

Muhtasari

• Msanii na mfanyibiashara KRG The Don amewajibu wanamuziki wa kundi la Mbogigenje akisema kwamba wao ni wasanii wa kikawaida na wala hawezi bishana nao.

• Vilevile msanii huyo amesema kwamba hana muda wa kubishana na Mbogigenje akisema kwamba yeye ni msanii wa kimataifa anayeishi Kenya na kwamba viwango vyao ni tofauti sana

KRG
Image: Hisani

Msanii na mfanyibiashara KRG The Don amewajibu wanamuziki wa kundi la Mbogigenje akisema kwamba wao ni wasanii wa kikawaida na wala hawezi bishana nao.

Akizungumza na wanablogu kadhaa siku ya Jumanne, KRG amekashifu vikali madai kwamba aliwakosea heshima wasanii hao, akisema kwamba alikuwa na kila haki kupakia video ya wimbo waliofanya pamoja kwenye akaunti yake ya youtube kwa kuwa yeye ndiye aliyegharamikia maandalizi ya video hiyo.

Vilevile msanii huyo amesema kwamba hana muda wa kubishana na Mbogigenje akisema kwamba yeye ni msanii wa kimataifa anayeishi Kenya na kwamba viwango vyao ni tofauti sana.

Ameongezea kwamba mwelekezi wa video ya ngoma hiyo alikuwa ametoka ughaibuni na kwamba wasanii hao hawangeweza kumlipa kiasi cha pesa alichokihitaji.

Krg  amewarai wasanii hao wa muziki wa gengetone kutafuta meneja ambaye ana uelewa wa muziki iwapo wanataka kutasua katika muziki na hata kutengeneza hela nyingi kupitia vipaji vyao.

Aidha amesema kwamba iwapo Mbogigenje wanajiamini kuwa wao ni wakali zaidi yake, basi wajipange watoe ngoma siku sawa ili waone gani itakayofanya vizuri na kuwafikia mashabiki wengi.

Amewataka wasanii hao kujifunza kujenga uhusiano mzuri na wasanii waliwatangulia kwenyen gemu ili kujifunza mbinu tofauti za kujikuza katika sekta hiyo.