KRG The Don na Vincent Mboya wamaliza tofauti zao

Muhtasari

• Msanii wa miziki ya Dancehall, KRG The Don na mwanablogu Vincent Mboya hatimaye wamemaliza tofauti zao huku KRG akiahidi kumpa kazi.

• Vincent Mboya aliahidi kwamba hatomtusi tena na kwamba atajishugulisha na mishe za kumletea hela na kuboresha maisha yake.

Mboya, KRG, na Butita
Image: Facebook

Msanii wa miziki ya Dancehall, KRG The Don na mwanablogu Vincent Mboya hatimaye wamemaliza tofauti zao huku KRG akiahidi kumpa kazi.

Kupitia video iliyopakiwa katika akaunti ya YouTube ya mwanablogu Nicholas Kioko, Vincent Mboya alionekana akimuomba KRG msamaha kwa kile kinasemekana kuwa kumharibia jina msanii huyo kwa mbambo asiyoyafahamu.

Vincent Mboya aliahidi kwamba hatomtusi tena na kwamba atajishugulisha na mishe za kumletea hela na kuboresha maisha yake.

Vilevile ,Mboya alisema kwamba yupo tayuari kumsamehe mcheshi Eddie Butita akisema kwamba hataki chuki na mtu yeyote.

KRG ambaye alikuwa amechoshwa na vita vya mara kwa mara alimuambia chipukizi huyo kwamba siri ya kufanikiwa sio kuwapiga vita walio mbele yake kimafanikio bali ni kuwatafuta ili wampe siri ya kufikia malengo yake.

Mwanamuziki huyo almaarufu Bughaa alijitolea kumpa kazi Mboya katika kampuni yake iliyoko katika eneo la Kiserian ambapo atakuwa anamlipa mshahara wa shilingi elfu hamsini kila mwezi.

Tayari Mboya ameanzisha biashara ya kuuza nguo zenye nembo yake akisema kwamba anatafuta mwekezaji ambaye atamsaidia kuboresha biashara hiyo na kuifanya kubwa zaidi.