Hajafanya poa,'KRG ashambuliwa na wanamitandao kwa kuwafokea Mbogigenje

Muhtasari
  • KRG ashambuliwa na wanamitandao kwa kuwafokea Mbogigenje
KRG the Don
Image: Facebook

Msanii na mfanyibiashara KRG The Don amewajibu wanamuziki wa kundi la Mbogigenje akisema kwamba wao ni wasanii wa kikawaida na wala hawezi bishana nao.

Akizungumza na wanablogu kadhaa siku ya Jumanne, KRG amekashifu vikali madai kwamba aliwakosea heshima wasanii hao, akisema kwamba alikuwa na kila haki kupakia video ya wimbo waliofanya pamoja kwenye akaunti yake ya youtube kwa kuwa yeye ndiye aliyegharamikia maandalizi ya video hiyo.

Vilevile msanii huyo amesema kwamba hana muda wa kubishana na Mbogigenje akisema kwamba yeye ni msanii wa kimataifa anayeishi Kenya na kwamba viwango vyao ni tofauti sana.

Baada ya wanamitandao kuona ujumbe wake KRG walijitokeza na kumshambulia msanii huyo kwa matamshi yake.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

steve_.g._official._: Nani huyo international ama nasoma vibaya😂

_sanboy._: Krg ndio nani actually😮😮😮😮 Mii najuwa mbogi Genje hapo pekee😂😂😂🚮🚮🚮

thee_nairobi_kid: Kiburi next level na hata hananga content 😂

starkid_musiq_ke: 😂😂😂😂😂😂 krg najua song yake moja tu nani juu ya mbuzi gang 😂

joybillie0: International artist na nywele amesongwa na mama mwende😂😂

worldbossofficiall: Ndo maana Kenya musics haifiki far…so much hatred among em’ 💔