Sijawahi kuchumbia mzungu yeyote- Vera Sidika aweka wazi

Muhtasari

•Vera alidai kwamba hata hajawahi kudhubutu kutafuta mzungu wa kuchumbia mitandaoni.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mtumbuizaji mashuhuri Vera Sidika ameweka wazi kwamba hajawahi kuchumbia mzungu.

Akishirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu, Vera alidai kwamba hata hajawahi kudhubutu kutafuta mzungu wa kuchumbia mitandaoni.

"Unauliza mtu asiyefaa. Sijawahi kuchumbia yeyote ama kuwa kwenye tovuti za kutafuta," Vera alijibu shabiki aliyeomba ushauri kuhusu mahali kwa kupata mzungu wa kuchumbiana naye.

Wanasoshalaiti wengi wamehusishwa sana na wazungu huku wengine wakionyesha wapenzi wao wazungu hadharani. Huddah Monroe ni mmoja wa wanasoshalaiti wa Kenya ambao wamewahi kuhusishwa na wazungu.

Kumekuwahi kutokea tetesi kuwa Vera pia amewahi kuwa kwenye mahusiano na wazungu ila amejitokeza kupuuzilia mbali madai hayo.

Mama huyo wa binti mmoja pia amefichua kuwa hajawahi kuishi nje ya nchi ya mipaka ya Kenya.

"Sijawahi kuishi nje ya Kenya. Sina lafudhi . Nazungumza kizungu fasaha tu," Vera alijibu shabiki aliyehoji Kizungu chake.

Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa nchi ya Afrika ambayo anaipenda zaidi na anamezea mate kutembelea ni Misri.