Sababu kuu ya rappa Sosuun kumcharaza msanii Vivianne

Muhtasari
  • Vivianne anasema alikasirika baada ya Sosuun kutokamilisha mradi waliokuwa wakifanya pamoja
Vivianne Kenya
Image: Facebook

Rapa wa Kenya Sosuun amemwacha Vivianne akiuguza majeraha baada ya kumshambulia.

Muimbaji huyo ambaye alofahamika sana kupitia kwa kibao chake cha 'Kufunikwa' alimvamia Vivianne katika kipindi cha Main Switch ambapo msanii huyo alikuwa na kipindi cha studio.

Katika video hiyo Sosuun mwenye hasira anaonekana akimthubutu Vivianne kumwambia mambo machafu ambayo alikuwa amemwambia mtandaoni ana kwa ana.

"Unanitukana kwenye mtandao kwa ajili ya nini? unataka nikuonyeshe ninachoweza kufanya? 'Alithubutu Sosuun kabla ya kwenda kushambulia Vivianne kwenye video iliyoenea mitandaoni.

Vivianne anasema alikasirika baada ya Sosuun kutokamilisha mradi waliokuwa wakifanya pamoja.

Asilimia kubwa ya wanamitandao wanadai kwamba wawili hao wanatafuta kiki kutokana na ugomvi wao kama wasanii wale wengine ambao wamekuwa wakitafuta kiki kutoka kwa mashabiki kabla ya kutoa kibao kipya.

Je kulingana na maoni yako wasanii hao wanatafuta kiki au la?