"Nipo single!" Mulamwah afichua uhusiano halisi kati yake na kipusa aliyetambulisha kama mpenziwe

Muhtasari

•Mulamwah amesema hakuna  uhusiano wa kimapenzi kati yake na mwanadada ambaye ameaminika kuwa mpenziwe  katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu ambacho kimepita.

•Ruth atakuwa msanii wa pili katika lebo ya mchekeshaji huyo na kibao chake cha kwanza kinatarajiwa kuachiwa Ijumaa.

Mulamwah na Ruth
Mulamwah na Ruth
Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji maarufu David Oyando almaarufu Mulamwah amefunguka ukweli kuhusu hali yake halisi ya mahusiano.

Mulamwah amefichua kwamba kwa sasa hachumbiani na yeyote huku akieleza kuwa hakuna  uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na mwanadada ambaye ameaminika kuwa mpenziwe mpya  katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu ambacho kimepita.

Baba huyo wa mtoto mmoja amemtambulisha Ruth kama msanii wake mpya katika lebo yake, 'Mulamwah Ent' na kudai hawajawahi kuwa wapenzi wala hawana mpango wa kuchumbiana.

"Kusema kweli hatujawahi kuchumbiana , na hatuna nia ya kuchumbiana.Haikueleweka. Kwa upande wangu mimi nabaki single na kuzingatia kazi zangu na miradi mingine iliyo mbele yangu," Mulamwah alitangaza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Ruth atakuwa msanii wa pili katika lebo ya mchekeshaji huyo na kibao chake cha kwanza kinatarajiwa kuachiwa Ijumaa.

Mulamwah alimtambulisha Ruthl kama mpenzi wake mpya takriban miezi mitatu iliyopita , siku moja tu baada ya kutangaza kutengana kwake na Carol Muthoni.