Shoga apata mtoto baada ya miaka mitatu, afurahia kuitwa baba

Muhtasari

• “Siku zote nilitaka kuwa baba, sikujua ni jinsi gani ningefanya hivyo. Hii ni kubwa! Ni wakati wa jamii kuona wanaume wa jinsia moja kama baba,” - Shoga Shaun Resnik

Shaun Resnik, shoga aliyepata mtoto
Shaun Resnik, shoga aliyepata mtoto
Image: Instagram

Ni furaha kwa mwanaume mmoja shoga kutoka taifa la Australia baada ya ndoto yake ya kuwa na mtoto na hatimaye kuitwa baba, kutimia.

Kulingana na Makala ambayo yamechapishwa katika jarida la Uingereza la Daily Mail, mwanaume huyo shoga kwa jina Shaun Resnik amekuwa kwa muda mrefu akitamani kuwa na mtoto licha ya msimamo wake wa kimapenzi kuwa shoga.

Jarida hilo linaeleza kwamba ilimchukua Resnik muda wa miaka mitatu na nusu kutimiza ndoto yake baada ya juhudi zake za kumtafuta mwanamke aliyekuwa tayari kuichukua mbegu yake na kumzalia mwana wa kurithi, kwa lugha ya kimombo ‘Surrogancy’ kugonga mwamba kwa mara kadhaa.

Daily Mail wanaripoti kwamba Resnik, 44, hatimaye alionekaniwa na nyota ya jaha baada ya kumpata mwanamke mmoja kwa jina la Bree aliyejitolea kuchangia yai lake la ovari kwa mwanamke mwingine kwa jina Carla Pincombe aliyekuwa radhi kumbebea mimba hiyo.

“Siku zote nilitaka kuwa baba, sikujua ni jinsi gani ningefanya hivyo. Hii ni kubwa! Ni wakati wa jamii kuona wanaume wa jinsia moja kama baba,” Daily Mail linaripoti vile Resnik aliiambia 7Life hapo awali.