Zuchu nambari 4 Afrika kwa wasanii wa kike wenye ufuasi mkubwa YouTube

Muhtasari

• Msanii Zuchu ameandikisha rekodi baada ya kuwa mwanamuziki waq kike wa nne katika bara la Afrika mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram.

Msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi
Msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi
Image: Instagram

Ninga wa muziki wa bongo fleva, mwanadada Zuchu kutoka rekodi lebo ya Wasafi amevunja rekodi nyingine baada ya kutinga kwenye nne bora ya wanamuziki wa kike kutoka barani Afrika wenye ufuasi mkubwa kwenye mtandao wa YouTube.

Zuchu ambaye ametajwa kama mwanamuziki anayekua kwa kasi ya ajabu kimuziki tangu kutambulishwa kwenye lebo ya Wasafi mnamo mwaka 2020 dunia ikiwa katika msukosuko wa janga la Corona amefikisha wafuasi milioni 1.9 kwenye YouTube na hivo kuwa mwanamuziki wa kike wa nne barani Afrika kuwahi kupiku idadi hiyo ya ‘subscribers’

Nambari moja inashikiliwa na mwanamuziki Sherine kutokea taifa la Misri ambaye mpaka sasa amejizolea wafuasi zaidi ya milioni 4.22 kwenye mtandao wa YouTube huku akifuatiwa na Zina Doudia kutoka Morocco akiwa na wafuasi milioni 3.04 naye malkia wa Afrobeats kutoka Nigeria Yemi Alade akiwa nambari tatu na wafuasi milioni 1.96 ambapo sasa Zuchu kutoka Tanzania akiwa na wafuasi milioni 1.9 akitazamia kumpiku Alade katika nafasi hiyo ya tatu.

Hongera sana Binti Khadija Kopa!