Baba Levo aahidi kufichua jina la 'mke' wa Diamond comment zikifika 2000 kwenye post yake Instagram

Muhtasari

• Mwanamuziki Baba Levo alisema yeye hajui kukaa na siri na kuahidi kwamba maoni yakipita elfu mbili kwenye instagram, ataliweka wazi jina la mpenzi wa Diamond Platnumz.

Diamond Platnumz, Zuchu
Diamond Platnumz, Zuchu
Image: Instagram, BAaba Levo

Mwanamuziki Baba Levo ambaye wengi wanamchukulia kama mtu wa mkono wa msanii Diamond Platnumz ametoa ahadi ya kuliweka wazi jina la ‘mke’ mtarajiwa wa msanii Diamond Platnumz iwapo ‘comment’ zitafika elfu mbili kwenye post ambayo amepakia kwenye Instagram yake.

Msanii huyo mwenye utata ambaye wengi wanafananisha tabia zake na zile za mtangazaji wa Clouds, Mwijaku kwa kuchamba watu bila woga anasema yeye mfumo wake haumkubalii kabisa kukaa na jambo rohoni kwani lazima alitame ndio awe huru.

Kulingana na Baba Levo, mfumo wake uko kama wa bahari haujui kukaa na kitu, Kitu kinatupwa sehemu moja kinasafirishwa kwa kusombwa kwenda sehemu ya pili, ndivyo alivyo Baba levo.

“Comment 2000 nilimwage jina… sikaangi na siri mimi,” aliandik Baba Levo akiambatanisha na picha ya bosi wake Diamond Platnumz.

Madai ya kuoa kwa Diamond Platnumz yaliwekwa wazi jana ambapo mama Dangote aliandika kwenye Instagram yake akimtaka mwanawe Diamond safari hii kutulia na kufanya harusi kabisa baada ya kumpata mwenza.

Kitendawili kikubwa ni pale kwa kumtaje mpenziwe Diamond ambapo licha na kwamba watu wengi tu wakiwemo watangazaji kutoka Wasafi kulizungumzia suala la Diamond kumpata mchumba na mpaka kudai ameoa kimya kimya, lakini fumbo kubwa linasalia kuwa jina na labda sura ya mrembo huyo mwenye bahati ya kunasa katika chambo ya mkurugenzi mkuu wa Wasafi.

Bado tunasubiri kama Baba Levo atatimiza ahadi yake ya kumwaga siri maana kwa upande wa comment mashabiki na wafuasi wanazidi kujikaza kurusha kadri ya uwezo wao ili kumjua shimeji mpya.