"Umekuwa baraka kwangu" Hamisa Mobetto amsherehekea bintiye kwa ujumbe maalum

Muhtasari

•Mobetto ameweka wazi kuwa binti huyo wake amekuwa baraka kubwa maishani mwake na kumtakia ulinzi wa Mungu.

•Mobetto  ana mtoto mwingine wa miaka minne, Dylan Abdul Naseeb kutoka kwa mahusiano yake yake na Diamond.

Hamisa Mobetto na familia yake
Hamisa Mobetto na familia yake
Image: INSTAGRAM// FANTASY FRANCIS

Binti wa msanii mashuhuri wa Bongo Hamisa Mobetto, Fantasy Majizzo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa hivi leo. (Aprili 10). Majizzo ambaye ni kifungua mimba wa Mobetto anasherehekea kutimiza miaka 7.

Hamisa Mobetto amezamia kwenye mtandao wa Instagram kumsherehekea binti huyo wake katika siku hiyo maalum kwake.

Katika ujumbe wake, Mobetto ameweka wazi kuwa binti huyo wake amekuwa baraka kubwa maishani mwake na kumtakia ulinzi wa Mungu.

"Kheri njema za siku ya kuzaliwa kwa binti wangu wa miaka 7 Fantasy Francis. Umekuwa baraka kwangu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kila siku kwa sababu yako. Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda mwanangu," Mobetto amemwandikia bintiye kwenye Instagram.

Mpenzi huyo wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz pia amemhakikishia binti yake kuwa anampenda sana.

Fantasy ni mtoto wa kwanza wa Mobetto kutoka kwa mahusiano yake ya kitambo na mfanyibiashara mashuhuri wa Tanzania, Francis Majizzo.

Mobetto  ana mtoto mwingine wa miaka minne, Dylan Abdul Naseeb kutoka kwa mahusiano yake yake na Diamond.