Fahamu faida za kuoa, kuolewa na kuishi katika maisha ya ndoa, raha sana!

Muhtasari

• Maisha ya ndoa yana faida nyingi kwa mfano walio katika ndoa huishi miaka mingi, huwa hawapatwi na magonjwa ya kawaida kama homa kwa urahisi, wana amani na utulivu wa nafsi na kihisia zaidi.

• Pia, watu walio katika ndoa hawana matatizo ya msongo wa mawazo na unyongovu.

Image: THE STAR

Bila shaka maisha ya sasa yanatofautiana kwa asilimia kubwa na maisha ya kitambo enzi za wazazi na mababu zetu.

Wataalam wa masuala ya maisha ya ndoa wanahoji kwamba zipo sababu nyingi tu zinazofanya watu wengi sasa hivi kuchukua mud asana kabla ya kuingia kwenye ndoa, sabau zenyewe zikiwemo ugumu wa maisha ambapo watu wanataka kwanza kujikimu kimaisha na kujitosheleza kabla ya kutafuta mwenza, hili huwakumba hasa wanaume.

Sababu ya pili ni kwamba wengi wanataka kwanza kukimbizana na ndoto za kitaaluma kabla ya kuingia kwenye ndoa, kwa dhana kwamba mtu ukishaingia katika ndoa basi huwezi pata nafasi kubwa ya kuiendeleza taaluma yako kwa sababu maisha ya ndoa yatakuhitaji zaidi na usipokuwa imara basi moja litakuponyoka, kati ya ndoa au taaluma. Hili nalo huwakabili sana wanawake.

Sababu ya tatu pia ambayo ni kigezo kikubwa ni kwamba wengi wanahofia kuingia katika maisha ya ndoa kutokana na kile wanaona kinawasibu wanandoa wengi, huku mijadala na habari za kutalikiana kwa wanandoa zikiwa ndio habari ya mjini katika maisha ya sasa.

Lakini licha ya haya yote, bado wataalamu wa afya wanahoji kwamba kuwa katika maisha ya ndoa au mahusiano kuna faida zake nyingi tu kiafya.

Kulingana na utafiti uliochapishwa katika tovuti moja humu nchini, maisha ya ndoa yana faida nyingi kwa mfano walio katika ndoa huishi miaka mingi, huwa hawapatwi na magonjwa ya kawaida kama homa kwa urahisi, wana amani na utulivu wa nafsi na kihisia zaidi kuliko watu wasiokuwemo katika mahusiano na ndoa.

Utafiti huo unazidi kueleza kwamba hata kitendo cha kuushika mkono wa mpenzi wako tu basi uwezekano wa kupatwa na shinikizo la damu hupungua kwa asilimia kubwa. Kuna visa vichache sana vya kujiuwa kwa watu walioko katika ndoa kuliko wale wasiokuwepo ndoani.

Pia, watu walio katika ndoa hawana matatizo ya msongo wa mawazo na unyongovu na iwapo matatizo haya hutokea japo kwa nadra basi wao hupona na kupata nafuu kwa haraka na iliyo imara kuliko wale waliotengana ama wasio katika ndoa.

Nakushangaa wewe unayesoma Makala haya na huna mpango wa kuingia katika ndoa kwa dhana kwamba wanaume wote ni umbwa ama wanawake wote wana utoto. Shauri yako!

Image: THE STAR
Image: THE STAR