Dufla azungumzia madai kuwa ndiye baba ya bintiye Sonnie, asema yupo tayari kumchukua

Muhtasari

•Dufla alidai yupo tayari kumsaidia mtoto huyo pamoja na mamake baada ya Mulamwah kuibua madai kuwa sio wake.

•Hivi majuzi Mulamwah alishangaza wengi baada ya kukana kuwa baba mzazi wa mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake.

Image: INSTAGRAM// DUFLA DILIGON, CAROL MUTHONI

Mwimbaji wa Dancehall Dufla Diligon amejitokeza kuzungumzia madai ya kuwa baba mzazi wa mtoto wa aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah, Carrol Sonnie.

Akizungumza katika Mahojiano na Eve Mungai, mwanamuziki huyo alisusia kukiri wala kupuuzilia mbali madai ya kuhusika na ujauzito uliopelekea kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Dufla amedai yupo tayari kumsaidia mtoto huyo pamoja na mamake baada ya Mulamwah kuibua madai kuwa sio wake.

"Sitaki kujibu kama ni wangu. Lakini mimi nipo tayari kumchukua nimsaidie pamoja na mama yake. Juu nimeona Mulamwah amechanganyikiwa. Nilikuwa nishapanga vile nitaenda tuzungumze na Carol tujue vile tutamaliza hayo mambo," Dufla alisema.

Mwanamuziki huyo aliweka wazi kuwa yeye na mpenzi huyo wa zamani wa Mulamwah wamekuwa marafiki kwa muda.

Alidai yupo tayari kumwajibikia mtoto huyo wa miezi saba hadi akue baada ya kuona aliyeaminika kuwa baba mzazi tayari amejitenga naye

"Kwa kuwa babake amesema sio wake, mimi nitamchukua. Nitamchukua kwa sababu Carol ni rafiki yangu. Mimi nitamchukue nimtunze na akuwe mtoto mkubwa. Niliona picha zake, yeye ni mtoto mrembo," Alisema.

Hivi majuzi Mulamwah alishangaza wengi baada ya kukana kuwa baba mzazi wa mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake.

Wanamitandao wameendelea kutoa hisia tofauti kufuatia madai hayo, baadhi wakimkosoa huku wengine wakionekana kumtetea mchekeshaji huyo.

Muthoni akiwa kwenye mahojiano na Massawe Jappanni mapema mwaka huu alisisitiza kuwa mtoto ni wake na Mulamwah. Alitangaza yupo tayari kwa vipimo vya DNA kufanyika iwapo itabidi.