"Huo ni usherati!" Jemutai alalamika baada ya Hamo kudai anataka nyumba ya kutulia peke yake

Jemutai alitilia shaka mpango huo.

Muhtasari

•Jemutai alitilia shaka mpango huo na kulalamika kuwa ni dalili ya mtu anayekusudia kujitosa kwenye uasherati.

•Hamo alitetea mpango wake huku akisisitiza kuwa anahitaji mahali ambapo anaweza kutulia bila usumbufu wowote.

Image: FACEBOOK// JEMUTAI

Mchekeshaji Herman Kago almaarufu Profesa Hamo amejipata upande mbaya wa mkewe wa pili Jemutai baada ya kudai anataka kusaka nyumba ya kutulia pekee yake.

Katika video ambayo Hamo alipakia Instagram, Jemutai alisikika akitilia shaka mpango huo na kulalamika kuwa ni dalili ya mtu anayekusudia kujitosa kwenye uasherati.

Hamo alisema alipata wazo la kujitafutia nyumba yake pekee baada ya kutazama video ya mwanadada anayedai kuwa kuishi nyumba tofauti na mumewe.

"Tulikuwa tunatazama video ya Steve Harvey saa hii. Kuna mwanadada huyu ambaye anasema anataka kuwa kwenye ndoa lakini aishi nyumba tofauti na mumewe. Niko na swali kwako (Jemutai) kwa kuwa nadhani ni sisi wote ni watu huru na tunaishi katika nyakati hizi mpya, je unajua 'Happy House'? Ni kanyumba kangu kama mwanaume mahali ambapo nitakuwa naenda kutulia.. " Hamo alisema kabla ya mkewe kumkatiza .

"Huo ni usherati,hakuna kupumzika, kupumzika ni nini?  si uende spa. Ati Happy House! " Jemutai alilalamika.

Hamo aliendelea kutetea mpango wake huku akisisitiza kuwa anahitaji mahali ambapo anaweza kutulia bila usumbufu wowote.

Yote tisa, ni bayana kuwa Jemutai hakukubaliana kabisa na mpango huo wa baba huyo wa watoto wake wawili.

Wachekeshaji hao wawili wa Churchill Show wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu na hata kubarikiwa na watoto wawili pamoja.

Mahusiano yao hata hivyo yalijulikana hadharani mwaka jana baada ya Jemutai kuzua madai kuwa mpenziwe hajakuwa akiwajibikia watoto wao.

Wawili hao walizozana kwa muda kati ya mwezi Aprili na Mei kufikia hatua ya Hamo kuagiza vipimo vya DNA.

Licha ya yote wapenzi hao waliweza kupatana hatimaye na kusuluhisha migororo yao. Mwezi Julai walianza ujenzi wa nyumba yao.