Mwanaume, 57, agundua wanawe 5 si wake baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 20

Mwanaume huyo alidhibitisha hili baada ya kufanay uchunguzi wa DNA

Muhtasari

• Baada ya kupigwa butwaa, watu walimshauri kuvumilia na kuwa "mwanaume kamili"

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Image: THE STAR, MOSES SAGWE

Mwanaume mmoja anayejulikana kama Elder Henry Shield kwenye mtandao wa Facebook amepakia habari moja ya kusikitisha na kutamausha kwa viwango sawa kuhusu mwanaume mmoja ambaye amepatwa na mshtuko wa karne.

Kulingana na taarifa hiyo, mwanaume mwenye umri wa miaka 57 ambaye alikuwa amedumu kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 20 alipatwa na mshtuko baada ya vipimo vya DNA kuonesha kwamba watoto wake 5 si wake tena kwa damu.

Taarifa hiyo iliibua mjadala mkali kutoka kwa wanamitandao haswa ikizingatiwa kwamab siku hizi kusalitiana katika mapenzi ni suala lenye mjadala mkali sana huku kila jinsia ilitupa lawama kwa jinsia nyingine kwamab wao ndio wameshikilia dhahabu katika kusaliti na kuchepuka.

Mwanaume huyo baada ya kuwekeza muda wake na mali yake kweney ndoa zaidi ya miaka 20 na watoto 5 juu, inakuja kuvunjika tu kwa kugundua kwamba hana uhusiano wowote wad amu ya kiukoo na familia aliyokuwa akijitoa kwa hali na mali akijua kuwa ndio warithi wake.

Inaumaje hiyo!

Baada ya kugundua hilo na kupigwa na butwaa ya moto, msimulizi alisema kwamab watu wa familia kutoka upande wa kikeni walichukulia poa na kumshauri kutohofu na kuwa kama mwanaume kamili asiyejali. Swali ni je, anaanzaje?

“Mwanaume ana umri wa miaka 57, alifanya uchunguzi wa DNA kwa watoto wake wote 5 na hakuna mtoto ambaye alikuwa wake. Alikuwa ameoa kwa miaka 20. Wanamwambia “kuwa mwanamume.” Sawa,” Elder Henry Shield alieleza.

Watu waligadhabishwa sana na taarifa hii ambapo mjadala mkali ulizuka, wengi wakimtetea mwanaume kwa kuchukua hatua ya kuenda DNA na wengine wakitaka kujua kulichomsukuma mpaka kufikia hatua hiyo yenye ukweli usiobeta, japo alienda kwa kuchelewa kweli!

“Awe mwanaume, basi!, hiyo ndio jamii tunajikuta baadhi ya wanawake ni zaidi, zaidi ya kuwa wabaya. Unategemea awaue hao watoto au vipi,” mwingine alisema.

“Alijisababishia matatizo yote hakupaswa kufanya ule uchafu unaoitwa DNA isipokuwa mtu anaburuza watoto naye,” Mmoja alishauri.