"Atwoli ameepa kuapishwa kwa Ruto" Watu wasema akiondoka kwenda London na Mkewe

Mwanahabari Mary Kilobi alipakia picha akidokeza kwamba wameondoka kwenda London kwa majukumu ya kimataifa.

Muhtasari

• “Zoea hiyo sauti, kwani hamujaalikwa shughuli ya kuapishwa dada? Safari njema lakini,” Dah Frii aliandika.

Francis Atwoli na mkewe mdogo Mary Kilobi wakiwa ndani ya ndege
Francis Atwoli na mkewe mdogo Mary Kilobi wakiwa ndani ya ndege
Image: Instagram

Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli mweney umri wa miaka 72 ameondoka nchini kuelekea London Uingereza na mkewe mdogo mwanahabari Mary Kilobi.

Taarifa za kuondoka kwao nchini kuenda kujivinjari Uingereza ziliwekwa wazi na Kilobi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kilobi alipakia msururu wa picha wakiwa na kipenzi chake kwenye ndege akisema kwamba ni majukumu ya kitaifa yaliita na ikabidi wapenzi hao kuambatana huku akidokeza kwamba wanaelekea Uingereza.

“Wakati majukumu ya kimataifa yanaita, tuwekeeni mazuri,” Kilobi aliandika.

Wengi walishindwa kujua mara moja ni majukumu gani hayo ya kimataifa yamewaita huku wengine wakimtania Atwoli kwamba ameenda kumuomboleza malkia Elizabeth wa pili aliyefariki juzi kati akiwa na miaka tisini na sita.

Wengine pia walimtania kwamba anatoroka ili kutohudhuria kuapishwa kwa rais Ruto Septemba 13, Jumanne ijayo, haswa ikizingatiwa kwamba Atwoli alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa hawaamini kabisa kama Ruto angekuwa Rais.

Mkongwe huyo ambaye amehudumu kama katibu wa chama cha wafanyikazi nchini kwa miaka mingi hadi aliwahi nukuliwa akiwaambia Wakenya kuanza kuzoea sauti ya kinara wa Azimio Raila Odinga kwani ndiye atakuwa rais.

Juzi Atwoli amemeza kiburi na majiambo yake na kukubali kwamba wao kama Azimio walikuwa hawaamini Ruto angeshinda kumbe kiongozi huyo wa UDA alikuwa mjanja kisiasa na kuwashinda, aliwataka Wakenya kujimwaya nyuma ya Ruto ili kumwezesha kutimiza manifesto yake ya Bottoms Up.

“Zoea hiyo sauti, kwani hamujaalikwa shughuli ya kuapishwa dada? Safari njema lakini,” Dah Frii aliandika.

“Mzee amekimbia kuapishwa,” Keith Sikobe alitania.

“Mliona kuenda kuombolezac daraja la London lililoporomoka ni muhimu kuliko kuhudhuria kuapishwa kwa rais,” Mwingine aliandika.