MACHOZI

Stivo Simple Boy atemwa na Malkia

Mally alisema kwa sasa yuko huru kuchumbiana tena.

Muhtasari

•Alisema kujihusisha kwake na Stivo kulikusudiwa kuwapata wafuasi zaidi kwenye mitandao yao ya kijamii.

•Alikanusha kuwahi kuolewa kabla ya kuchumbiana na Sivo baada ya wanaume wawili kudai alikuwa na mahusiano nao hapo awali.

Mally Malkia
Mally Malkia
Image: HISANI

Mpenzi wa Stivo Simple Boy Mally Malkia amesema kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na mwanamuziki huyo wa genge.

Akiongea kwenye mahojiano na YouTuber Princess Rozyline, Mally alifichua kuwa Stivo alimpa bega la kuegemea walipokutana Mombasa miezi michache iliyopita.

Alisema alikuwa amemwacha mpenzi wake wa zamani kwa sababu ya tabia zake mbaya wakati Stivo alipomjia maishani mwake.

Mally aliongeza kuwa hakuvutiwa na mwanamuziki huyo mara ya kwanza walipokutana, lakini alijikuta akiingia kwenye mapenzi kadri muda ulivyokuwa unakwenda.

Alisema kujihusisha kwake na Stivo kulikusudiwa kuwapata wafuasi zaidi kwenye mitandao yao ya kijamii.

Mally alisema kwa sasa yuko huru kuchumbiana tena na kufichua kuwa anammezea mate mwimbaji wa Nigeria Ruger.

"Kusema kweli, mimi niko peke yangu. Sichumbii! Ilikuwa showbiz tu na hiyo imekwisha sasa," alisema.

Alikanusha kuwahi kuolewa kabla ya kuchumbiana na Stivo baada ya wanaume wawili kudai alikuwa na mahusiano nao hapo awali.

Wakati huo huo, Stivo Simple Boy amefuta picha za Mally kwenye vishikizo vyake vya kijamii.

"Inauma lakini sina budi ila kukubali ukweli," Stivo alichapisha.