Mlinzi amtimua mwanatiktoker kwa kujaribu ku'shoot' video sokoni

Kijana alipandwa na mori alipokatizwa kufanya video hiyo ya kuchekesha na mlinzi.

Muhtasari

• Alijaribu kudinda kutoondoka eneo hilo kama alivyoagizwa lakini jambo hili lililomfanya mlinzi huyo kumfukuza kwa nguvu.

Image: Tiktok

Mwanatiktok mmoja alizua kioja sokoni baada ya kufukuzwa na mlinzi mwenye bunduki alipojaribu kutengeneza klipu ya kuchekesha sokoni. 

Kijana huyo alipofika sokoni alianza kurap kwa sauti ya juu  jambo lililomghadhabisha  mlinzi wa usalama aliyekuwa karibu kumgonga na kumfukuza.

Tukio hili liliwavutia wapita njia waliojionea drama baina ya mlinzi huyo na kijana barobaro. Kijana alipandwa na mori alipokatizwa kufanya video hiyo ya kuchekesha.

Alijaribu kudinda kutoondoka eneo hilo kama alivyoagizwa. Kutotii kwake kulimfanya mlinzi huyo kutumia nguvu kumwondoa sehemu ile.

Kijana huyu alionyesha kutokuwa na heshima kwa mlinzi kwa jinsi ambavyo alivyomrushia mikono mlinzi huyo aliyekuwa na ghahabu.

Video hiyo ambayo ilikuwa imepata watazamaji zaidi ya laki 9 iliwafanya watumiaji wa mitandao kutoa hisia mseto huku baadhi wakidhihirisha kutopendezwa kwao na kitendo cha kijana yule huku wengine wakifurahia kwa kucheka.

''Mbona unatoroka, endelea kusema yo yo yo yo'' mmoja wa watumizi wa mitandao alimtania.

''Lakini ilikuwaje video ya kwanza kwa sababu hii imesambaa sana'' mwingine alitania pia.

Wakati huo huo inaaminika kwamba kijana huyo alijaribu kumtania mmoja wa walinzi hao kutoka Nigeria  alipompa barua kisha kutoroka.

ingawaje barua hiyo haikutambulika ilivyokuwa imeandikwa ila mlinzi huyo wa usalama  alipoisoma, alitazama alikokwenda kijana.

Maneno yaliyowekwa kwenye video hiyo yalisema kwamba kijana huyo alilazimika kumsihi askari huyo baadaye.