Jalong'o aombwa kuwasamehe waliokuwa wafanyikazi wake

Wengi walidhani mbunge huyo anatafuta kiki baada ya wawili hao kuiba pesa na Jalang'o akapaza sauti.

Muhtasari
  • Mmoja wao kwa Jina Eli hivi majuzi amekuwa akiomba Jalang'o amwajiri tena, kwani wakati fulani alishtumu shetani kwa kuwajaribu

Ni miezi kadhaa imepita tangu mbunge wa Lang'ata Felix Odiwuor alipowatimua wafanyikazi wake wawili wa nyumbani baada ya kumwibia pesa.

Wengi walidhani mbunge huyo anatafuta kiki baada ya wawili hao kuiba pesa na Jalang'o akapaza sauti.

Miezi kadhaa baadaye ikawa kweli ingawa wawili hao walirudisha kiasi cha pesa, walifukuzwa kazini.

Mmoja wao kwa Jina Eli hivi majuzi amekuwa akiomba Jalang'o amwajiri tena, kwani wakati fulani alishtumu shetani kwa kuwajaribu.

Leo akiwa kwenye machapisho yake ya kawaida kwenye mitandao ya kijamii, Eli alisasisha video ambayo alikuwa akitengeneza nyumba ya udongo.

Kwenye video hiyo Eli anasikika akiomba Jalang'o amfikirie upya na kumwajiri tena akisema kuwa maisha ya kijijini yamekuwa magumu.

Wanamtandao walioonekana kumuonea huruma Eli walimtambulisha Jalang'o wakimwomba afikirie upya na kumrejesha Eli kazini.

Walibainisha kuwa licha ya kukatishwa tamaa, Jalang'o anafaa kufikiria upya uamuzi wake thabiti na kumrejesha Eli kazini.

Hizi haapa baadhi ya jumbe za wanamitandao;

lenana_g@: jalangoo tulikupee kazi sasa samehe eli arudi kazi

mwaikadu: Mhesh @jalangoo One more chance

lagat_ezra: @jalangoo do something mhesh.i