"Hivi mnajua niliyoyapitia!" Harmonize aweka wazi hali yake ya sasa ya mahusiano

"Msijali, hivi karibuni nitapata mtu na mtamjua!!," alisema.

Muhtasari

•Harmonize alisema kwa sasa anajipatia muda usiojulikana wa mapumziko kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mapya.

•Harmonize sasa amebainisha kuwa kuna nafasi kubwa ya upendo ndani ya moyo wake uliovunjika mwaka jana.

Bosi wa Konde Music Worldwide, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amethibitisha kuwa hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa.

Katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatano, Konde Boy alisema kwamba kwa sasa anajipatia muda usiojulikana wa mapumziko kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mapya.

"Msijali, hivi karibuni nitapata mtu na mtamjua!!," alisema.

Staa huyo wa Bongo alidokeza kwamba alipitia masaibu mengi mno wakati akiwa katika mahusiano yake ya awali.

Alionekana kuwakashifu wakosoaji na kuwataka wasite kumhukumu kwa kuwa hawana ufahamu wowote wa aliyopitia.

"Wasikuone na kidem tuu!! Hivi mnajua niliyo yapitia," aliandika.

Muigizaji Frida Kajala Masanja alithibitisha kutengana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchumbiana naye kwa takriban miezi saba. 

Ingawa hakuweka wazi kilichowatenganisha, alibainisha kwamba hakubeba kinyongo dhidi ya mwimbaji huyo licha ya mahusiano kugonga mwamba.

Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.

Mama huyo wa binti mmoja aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano kusambaratika.

Harmonize sasa amebainisha kuwa kuna nafasi kubwa ya upendo ndani ya moyo wake uliovunjika mwaka jana.

"Upendo una nafasi kubwa sana kwenye kichwa changu. Ndio maana napenda watu kuliko pesa. Unaweza hisi mjinga flani. Kwa sasa niko single. Nataka tu kuchukua muda wangu Inshallah," alisema Jumatano.

Mwezi uliopita, alidaiwa kutoka kimapenzi na mshiriki wa zamani wa Big Brother Africa Feza Kessy. Baadaye hata hivyo ilibainika alikuwa akitafuta kiki tu baada ya kumshirikisha kipusa huyo kwenye wimbo 'Wote'