Mama na dadake Diamond wadaiwa kujihusisha na vijana wadogo 'vibenten', dadake ajibu

"Una ubora gani kila siku unaachika kazi kulea vibenten wewe na mama yako,"

Muhtasari

•Esma ambaye ni dada mkubwa wa staa huyo wa Bongo alisherekea kufikisha miaka thelathini na saba humu duniani.

•Esma  hakafutilia mbali tetesi za mwanadada huyo bali alijigamba kwa kuweza kufikia hatua ya kuvishwa pete.

katika picha ya maktaba
Mama Dangote, Diamond Platnumz, Esma Platnumz katika picha ya maktaba
Image: INSTAGRAM// ESMA PLATNUMZ

Siku ya Alhamisi, Februari 2, dada ya mwimbaji Diamond Platnumz, Esma Khan aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Esma ambaye ni dada mkubwa wa staa huyo wa Bongo alisherekea kufikisha miaka thelathini na saba humu duniani.

Katika siku hiyo maalum kwake, mama yake Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote alikiri kujivunia yeye. Mama Dangote alisema anajivunia kumzaa na kumlea Esma huku akimtakia maisha marefu zaidi.

"Sina chakuandika, ila najivunia kukuzaa na kuwa Mama Bora kwako Esma, @_esmaplatnumz nakutakia maisha marefu yenye baraka tele kwenye kuongeza mwaka mwingine," aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Katika jibu lake, Esma alimshukuru mzazi huyo wake na kudokeza kuwa ameiga mfano wake katika kuwalea binti zake.

Kama kawaida, wanamitandao wengine pia walitoa maoni kwenye chapisho hilo. Mwanadada mmoja alinasa umakini wa Esma alitilia shaka ukamilifu wake akidai kuwa hangeweza kutulia katika ndoa bali, pamoja na mamake, walijihusisha na wanaume wadogo tu.

"Una ubora gani kila siku unaachika kazi kulea vibenten wewe na mama yako," @lynne_mtandi alimwambia Esma.

Mama huyo wa watoto watatu hakafutilia mbali tetesi za mwanadada huyo bali alijigamba kwa kuweza kufikia hatua ya kuvishwa pete.

"Ndo majaaliwa yangu bora na ninaolewa kuna watu wanaachika bila hata pete kuvishwa kila siku," alijibu Esma.

Mtumizi mwingine wa Instagram alimshtumu Esma kwa kuwa mfano mbaya kwa binti zake kuhusu suala la ndoa.

"Ukweli amekuwa mama Bora lakini hana mfano mzuri ktk mabinti zake mama asiye na Ndoa ni jambo Dogo lakini ni kubwa kwa mafunzo kwa watoto tunachukulia poa lakini sivyo address ina umuhimu sana tena yeye Kazaa mabinti,"@nashe_ngena alimwambia.

Kufikia sasa, dada huyo wa Diamond anadaiwa kuondoka kwenye mahusiano kadhaa ikiwemo ndoa mbili halisi.

Ndoa ya mwisho ya Esma aliolewa kama mke wa tatu kwa mfanyabiashara wa Tanzania, Maulid Msizwa mwaka wa 2020 lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miezi mitatu pekee. Kwa sasa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano mapya.