Mwanablogu aomba kuchangiwa nauli kwenda ofisi za Instagram USA kufunguliwa akaunti

Mwanablogu aomba mchango wa pesa kusafiri kwenda ofisi za Instagram USA kuomba kufunguliwa akaunti zake zilizofungwa.

Muhtasari

• Alisema nia yake ni kulainisha mambo na kampuni ya Meta huko Marekani ili kupata mwafaka na kufunguliwa akaunti hizo zilizofungwa mwaka mmoja uliopita.

Mwanablogu CarryMastory kutoka Tanzania
Mwanablogu CarryMastory kutoka Tanzania
Image: Screenshot

Mwanablou wa udaku kutoka nchini Tanzania Carry Mastory ameweka bango kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa watu kumpa mchango wa pesa kufanikisha safari yake kuelekea Marekani.

Mastory alisema kuwa nia yake ya kwenda Marekani ni moja tu – kufika makao makuu ya kampuni ya Meta inayojumuisha mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp, makao ambayo yanatajwa kuwa katika jimbo la California.

Mwanadada huyo mmbea alisema dhima yake kubwa ni kukutana na uongozi wa kampuni hiyo ili kufanya mazungumzo nao kumfungulia akaunti zake mbili za Instagram zilizofungwa ziliwa na wafuasi wengi.

Nina masikitiko makubwa kuwataarifu Umma ni mwaka sasa kurasa zangu mbili za Instagram Carrymastory 2.7Millions followers na Carrymastorytv 689k zifungiwe na za wengine wengi ambao tunawajua. Baada ya kukaa kikao na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania (Jumikita) tumefikia muafaka kuwa Carrymastory nimefanya kazi nyingi sana kwenye jamii na naamini watanzania wananipenda, Ni muda sasa wa Kutembelea makao makuu ya Instagram Kwanza kutengeneza ukaribu na mahusiano mazuri kati ya kampuni ya Meta na sisi wanamitandao ya kijamii,” Mastory aliandika.

Kwenye tangazo hilo, aliambatanisha namba yake ya simu ambayo pesa zitatumwa pamoja pia na akaunti zake za benki.

“Tangazo hili ni kuomba kufunguliwa akaunti zetu zilizofungiwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamewekeza Nguvu na Muda wao kuzimwa kimakosa. Tunaomba mchango wako wewe mdau unayependa mitandao ya kijamii. Changia Carrymastory kwenda Makao makuu ya Google Facebook, Instagram kwaajili ya kutengeneza Mahusiano mazuri na Meta, kama wanamitandao ya kijamii. ”