Wasafi na Mziiki wameungana kuchezea maisha yangu-Harmonize alia

Harmonize amesema kwamba anahitaji malipo yake ili aweze kusaidia familia yake kama vile wasanii wenzake wanavyofanya.

Muhtasari
  • Msanii huyo amesema kwamba hajatendea mabaya lebo hizo mbili, bali shida ni pale anapotaka malipo ambayo hajawahi kukusanya au kupata baada ya nyimbo zake

Staa wa bongo Harmonize kwa mara nyingine kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameshambulia lebo za muziki za Wasafi na Muziiki.

Msanii huyo amesema kwamba hajatendea mabaya lebo hizo mbili, bali shida ni pale anapotaka malipo ambayo hajawahi kukusanya au kupata baada ya nyimbo zake.

Harmonize amesema kwamba anahitaji malipo yake ili aweze kusaidia familia yake kama vile wasanii wenzake wanavyofanya.

"I need 5 Royals Wasafi na Mziiki wameshirikiana kuchezea maisha yangu, na sikuwafanyia chochote ubaya unaanza pale mtu unapotaka jasho lako ili uisaidie familia yako kama ao wanavyofanya 

Unaweza aje kukaa na haki ya mtu wakati anaipambania miaka 3 unachukua wewe huogopi hata laana ya Mungu

Big Bro Mwanafa,hongera na nakuomba uanze na hili, mama anajua wewe ni suluhu nyingine,BASATA na KOSOTA  sijawahi kusanya malipo yangu kwa miaka 3."

Haya yanajiri siku chache baada ya msanii huyo kutishia kuacha muziki baada ya madai ya kupokea hujuma kutoka kwa tasnia ya burudani.

Harmonize alisema yuko tayari kufa akipigania haki zake pamoja na wasanii wenzake mradi awe ameacha utajiri mkubwa kwa binti yake.

Baadhi ya madai ambayo aliibua ni pamoja na:-

  • Sijapokea hela za uchapishaji muziki kwa miaka 7
  • Kuna mtu anadai kumiliki miziki yangu inapochapishwa.
  • Kunyanyaswa na kudhalilishwa sana.
  • Nitakata ushirikiano na Mziiki nisipoelezwa ukweli.
  • Wazalishaji wamenyimwa haki ya kuchapisha ngoma.
  • Siogopi mtu mwingine ila Mungu na serikali
  • Nitafurahi nikifa leo na nimuache binti yangu tajiri
  • Ninapigania wasanii wengi wanaodhulumiwa.