"Niko single!" Mwimbaji Marioo afichua sababu ya kuachwa na mpenzi wake

Mwimbaji huyo alidokeza kuwa changamoto nyingi maishani zilimfanya mpenzi wake kutoroka.

Muhtasari

•Marioo aliachia toleo lake la wimbo wa Harmonize 'Single Again' ambapo alitumia maneno yake  kusimulia  jinsi alivyoishia kuwa single.

•Marioo aliweka wazi kuwa licha ya kutokuwa na mpenzi, amewahi kuwa kwenye mahusiano na si bikra.

Image: INSTAGRAM// MARIOO

Mwimbaji wa Bongo Omary Ally Mwanga almaarufu Marioo amedokeza kwamba hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa.

Siku ya Jumatano, mwanamuziki huyo mbunifu aliachia toleo lake la kibao kipya cha Harmonize 'Single Again' ambapo alitumia maneno yake mwenyewe kusimulia  jinsi alivyoishia kuwa single.

"Ooh kweli mimi ni single," aliandika.

Katika wimbo huo, Marioo aliweka wazi kuwa licha ya kutokuwa na mpenzi, amewahi kuwa kwenye mahusiano na si bikra.

Wakati huohuo, mwimbaji huyo alidokeza kuwa changamoto nyingi maishani zilimfanya mpenzi wake kutoroka.

"Nilikuwa na mtoto, nampenda kama mtoto,

Alinimalizianga uroto, wa moto

Nilikuwa na mtoto, mzuri kama mtoto

Changamoto kambeba," aliimba.

Harmonize aliimba wimbo 'Single Again' takriban miezi miwili tu baada ya uhusiano wake na Kajala kusambaratika.

Alitumia wimbo huo kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano huku akisema kuwa labda hakukusudiwa kupenda.

Mwezi uliopita, alidokeza kwamba ni vigumu kwake kujitosa kwenye mahusiano mengine kwa kuwa imekuwa vigumu kwake kumwamini yeyote.

Aidha, alidokeza kwamba wakati akiwa kwenye mahusiano yake ya awali alidanganywa sana na wapenzi ambao hakuwafichua.

"Kuna wasichana ambao wananipenda kabisa. Ni vigumu sana kwangu kumwamini mtu yeyote TENA!!! Ewe Mungu, NATAKA KUWA SINGLE MILELE . Siwezi kukubali uongo tena," Alisema staa huyo wa Bongo.

Wakati huo huo, mwimbaji huyo alidokeza kwamba alijitoa mali na hali ili kumridhisha mpenzi wake wa zamani.

Kufuatia hilo, hasidi huyo wa Diamond Platnumz aliwashauri wanaume kuzingatia kutengeneza pesa badala ya mapenzi.

Aliyekuwa mpenzi wake wa hivi majuzi, muigizaji  Frida Kajala Masanja alithibitisha kuvunjika kwa mahusiano yao mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchumbiana naye kwa takriban miezi saba.