Stivo Simple Boy afunguka kuhusu mkewe kuwa mjamzito

Simple Boy alimtambulisha Grace Atieno kama mkewe siku ya mazishi ya babake.

Muhtasari

•Stivo Simple Boy ameweka wazi kwamba habari kuwa anatarajia kupata mtoto na mke wake Grace Atieno ni uongo.

•Simple Boy alimtambulisha Grace baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy

Image: INSTAGRAM// STIVO SIMPLE BOY

Mwimbaji wa nyimbo za kufoka Stivo Simple Boy ameweka wazi kwamba habari kuwa anatarajia kupata mtoto na mke wake Grace Atieno ni uongo.

Kwenye mtandao wa Instagram, Simple Boy alibainisha kuwa aliibua madaihayo mnamo tarehe 1 Aprili, ambayo ni siku ya wajinga duniani.

"Jana ilikuwa tarehe 1 April siku ya uongo duniani,najua hamkumbui , nawapenda sana," alisema Simple Boy.

Simple alimtambulisha mpenzi wake siku ya mazishi ya babake nyumbani kwao katika eneo la Oyugis, kaunti ya Siaya.

Simple Boy alisema kuwa alikuwa na nia ya kumtambulisha  mpenzi wake kwa babake ila kwa bahati mbaya baba yake aliaga kabla ya hilo kufanyika.

Simple Boy alimtambulisha Grace baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy ambaye tangu kutengana kwao wamekuwa wakirushiana vijembe mtandaoni, Pritty Vishy akidai kuwa Grace si mke wa Stivo kwani wangekuwa wamefunga ndoa.

Baada ya Stivo kutangaza kuwa anatarajia mwana na Grace, Pritty Vishy, kwenye mtandao wa Instagram alidokeza kuwa anashuku kuwa ujauzito huo si wa Simple Boy.

"Nikisema mimba hiyo si yake mtasema kuwa nina wivu," alisema Vishy.