Mke afariki na kumuacha mume na watoto 2, apima DNA na kupata wote si wake!

Hata hivyo, baadhi walimshauri kuwalea wanawe kwani yeye ndiye msaada pekee uliosalia na hawamjui mzazi mwingine kando na yeye.

Muhtasari

• Roux ambaye alikuwa anaomba usaidizi alisema ana miaka 36 na marehemu mke wake alimuacha na watoto 2.

Kifaa cha kupima DNA nyumbani
Kifaa cha kupima DNA nyumbani
Image: Maktaba

Mwanamume mmoja kwenye mtandao wa Twitter amezua mjadala pevu bada ya kudai kwamba alipata pigo mara mbili kwa kipindi kifupi na kulazimisha kusalia na kovu zito moyoni mwake.

Mwanamume huyo anayekwenda kwa jina Barry Roux alisema kuwa pigo la kwanza lilikuwa ni kufiwa na mke wake na wakati bado hajakaa vizuri kutokana na kuomboleza, akapata pigo la pili kugundua kwamba watoto aliobaki nao si damu yake.

Roux ambaye alikuwa anaomba usaidizi alisema ana miaka 36 na marehemu mke wake alimuacha na watoto 2 lakini baada ya kuanya udhubutu wa kupima DNA, makubwa yalimkuta kiasi kwamba alihisi asingechukua uamuzi wa DNA kwani alipata watoto wake wote si damu yake.

“Mke wangu alifariki na kuniacha na watoto wawili lakini hivi majuzi nimegundua kwamba watoto si wangu baada ya vipimo vya DNA. Nina miaka 36 naomba ushauri wenu,” Roux aliandika katika Tweet hiyo ambayo imeenezwa pakubwa.

Kulingana na tweet hiyo ya Roux ambaye alionekana kujuta uamuzi wa kupima DNA, alishindwa nani angemjibu maswali kuhusu baba halali wa watoto ambao amekuwa akilea kwani tayari maskini mke wake alikuwa kehsatangulia mbele za haki.

Baadhi walimshauri kukubali hali na kuwalea watoto hao kwani yeye ndio msaada pekee kwao uliobaki na hio halitobadilika sababu hata akatuama vipi hawezi pata majibu anayotafuta kuhusu baba aliyewazaa.

Wewe ungemshauri vipi?