Mwanaume aghairi harusi baada ya kugundua mrembo wake alifanya mapenzi na Ex wake

Mrembo alisema alikwenda kumpelekea Ex wake barua ya mwaliko kuhudhuria harusi lakini akajikuta wamefanya mapenzi "kwa bahati mbaya".

Muhtasari

• Baada ya kumpa barua, Ex wake alimsihi kuketi waongee na akajikuta amelala huko na kufanya mapenzi naye usiku wote.

• Kumbe mpenzi wake alikuwa amedukuwa WhatsApp yake na alikuwa anafuatilia mazungumzo yao na siku moja alimuuliza.

• Papo hapo aliita wazazi wake mbele yake na kuwaamrisha kusitisha mipango yote ya harusi mara moja.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Mwanamké wa Nigeria ambaye alipaswa kuolewa tarehe 25 ya mwezi huu na mchumba wake wa muda mrefu amesalia akijifuta machozi baada ya mume wake mtarajiwa kughairisha mipango yote ya harusi.

Kulingana na hadithi iliyoenea kwenye mtandao wa Facebook, mwanamume huyo aligundua kwamba mwanadada huyo alimtembelea mpenzi wake wa zamani siku chache zilizopita huku mipango ya harusi yao ikiwa imeshika kasi.

Bibi harusi huyo mtarajiwa ambaye jina lake halikutajwa, alifikisha suala hilo kwenye kundi la Facebook na kutaka maoni ya wanachama wa kundi hilo.

Alisema alimtembelea tu mpenzi wake wa zamani ili kumpa kadi ya mwaliko kwenye harusi yake, lakini aliishia kulala huko na kujipata wameshiriki kitendo cha kuvunja amri ya saba kwenye amri kumi za Musa katika Biblia.

Kwa bahati mbaya kwake, mume wake mtarajiwa aligunduliwa kuhusu kitendo hicho baada ya kuingia kwenye Whatsapp yake. Baadaye mwanamume huyo aliagiza kwamba matayarisho yote ya arusi yasitishwe bila kukawia.

 

“Harusi yangu ya kitamaduni ni Mei 25 na harusi Mei 27. Mchumba wangu alighairi kila kitu kwa sababu nilimdanganya. Nilienda kumpa mpenzi wangu wa zamani Mwaliko wa harusi yangu. Nia yangu haikuwa kulala. Alianza kunisihi kwamba tuna mengi ya kuzungumza. Kwamba niruhusu tuzungumze sasa kwa kuwa bado sijaolewa.”

“Alinisihi nilale na nilifanya hivyo. Jambo moja linaongoza kwa lingine, tulijikuta tumeshiriki kitendo usiku wote. Sikumwambia mchumba wangu na hajawahi kunihoji kuhusu hilo. Bila kujua kwamba alidukua simu yangu na anasubiri muda atakaokuwa nami ili tuongee kuhusu hilo.”

“Aliniuliza nikadanganya. Kisha akatoa ushahidi. Hakukuwa na njia ya kutoka hivyo nikaanza kuomba msamaha. Mbele yangu, aliwaita wazazi wote wawili na kuwataka kufuta maandalizi yoyote ya harusi. Walipouliza kwa nini, aliwaambia nitawaeleza vizuri zaidi.”

"Aliniacha nyumbani kwake na kwenda hotelini na anarudi Abuja kutoka hotelini. Alimuagiza mlinzi wake wa getini ahakikishe naondoka kesho na nimshushie funguo za nyumba. Nimempigia simu zaidi ya mara 800, hachukui. Tafadhali naweza kufanya nini kurekebisha hili. Sitaki kumpoteza mtu wangu. Tunapendana sana. Nahitaji msaada, tafadhali. Moyo wangu dhaifu hauwezi kustahimili haya."

 

Ungemshauri nini?