Mama wa watoto 6 akiri 4 ni wa pasta, mmoja wa muuza nyama na mmoja ndio wa mumewe (video)

Watu waligawanyika kwa maoni kuhusu wa kulaumiwa kati ya mke, mume, pasta na muuza nyama.

Muhtasari

• “Niambie kitu ambacho sijui kuhusu wachungaji/watu wa Mungu waliosemwa huko Afrika!? Ni aibu sana jinsi walivyoendelea kufanya mabaya zaidi!” Mazie Chidiime.

Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Image: Forbes

Mwanamke mmoja amewashangaza wengi baada ya kuandamana na aliyekuwa mumewe kwenda katika kipindi kimoja cha redio na kumfunulia makombora ambayo mume huyo kwa njia moja au nyingine hakuwa tayari kupokea.

Kwa mujibu wa video iliypopakiwa katika mtandao wa X, awali wengi wakiujua kama Twitter kwa jina Oloye TD, mwanamke huyo bila kuonesha kujutia, alifichua mbele ya mumewe kwamba watoto 5 kati ya watoto 6 waliojaaliwa nao si wake.

Mama huyo aliyezungumza kwa lugha ya kiasili ambayo ilitafsiriwa kwa Kiingereza na mtumizi huyo wa Twitter alisema kwamba watoto 4 kati ya sita alizaa na mchungaji wa kanisa alilokuwa akishiriki, mmoja akazaa na muuza nyama na mwingine wa mwisho ndiye tu mtoto aliyezaa na mume wake.

“Kati ya Watoto Sita (6), Mchungaji wake ana wanne (4), mwanaume mwingine muuza nyama ana mmoja wakati mume ana (1) MMOJA tu💔Ni nini hasa kinatokea🙁” Oloye TD alitafsiri.

Baadhi ya watumizi wa X, walimhurumia mwanamume huyo huku wengine wakisema kwamba huenda kwa njia moja au nyingine alichangia mkewe kuchepuka na wengine kutupa lawama kwa mtumishi wa Mungu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

“Wanaume bado hawajatambua kuwa Wanawake wanachangia 90% ya shida tunazokabili maishani,” Charles Chinwe.

“Niambie kitu ambacho sijui kuhusu wachungaji/watu wa Mungu waliosemwa huko Afrika!? Ni aibu sana jinsi walivyoendelea kufanya mabaya zaidi!” Mazie Chidiime.

“Sio mcheshi hata kidogo, mwanamke huyu ni mbaya sana” Niki Abiola.