Mwanaume ampiga mama wa mpenziwe kwa 'kushindwa kuunga mkono uhusiano wao'

Kulingana na ripoti, hii si mara ya kwanza kwa kijana huyo kumshambulia mwanamke huyo kwa sababu tu haungi mkono uhusiano wake na binti yake

Muhtasari

• "Hii ni kwa sababu mwanamke huyo haungi mkono uhusiano wa bintiye na mvulana huyo,” ripoti hiyo ilisema.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Kijana mmoja amefanya jambo lisilofikirika kwa kumpiga mama mzazi wa mpenzi wake kwa kushindwa kuunga mkono uhusiano wake na bintiye.

Mama wa mpenzi wake alipata majeraha mabaya usoni, kichwani na sehemu nyingine za mwili kutokana na shambulio hilo.

Polisi wamearifiwa kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la Volta nchini Ghana, lakini familia ya mwathiriwa imeeleza kutofurahishwa na jinsi kesi hiyo inavyoendeshwa na imetishia kulipeleka suala hilo ngazi ya juu Zaidi, chombo cha habari cha ndani kiliripoti.

Mhasiriwa ambaye hali yake ya kifedha inamzuia kumudu uwakilishi wa kisheria, ameita kesi mahakamani na anawasiliana na wakili yeyote anayeweza kumsaidia kupitia mchakato wa kisheria.

Kulingana na ripoti, hii si mara ya kwanza kwa kijana huyo kumshambulia mwanamke huyo kwa sababu tu haungi mkono uhusiano wake na binti yake

“Simu ya kwanza ambayo nilikosa mapema leo asubuhi ilikuwa kutoka kwa jamaa wa bibi kwenye picha hii. Kwa sasa yuko hospitali kutokana na kushambuliwa na mpenzi wa bintiye ambayo si mara ya kwanza. Hii ni kwa sababu mwanamke huyo haungi mkono uhusiano wa bintiye na mvulana huyo,” ripoti hiyo ilisema.

Iliendelea: "Binti mkubwa aliripoti kesi kwa polisi na kesi iko mahakamani lakini familia haiwezi kumudu wakili na kesi hiyo ni kesi ya kijinga kwa sababu ya uhusiano wa mwanamume na polisi.

Wanahitaji wakili au mtu yeyote anayeweza kusaidia katika kesi hii.