Ukichumbiana na mwanamume mwaka 1 na hajakununulia gari, achana naye – Warembo washauriwa

“Kwa sababu kama mwanamume anakuthamini, ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja atakununulia gari. Njia ya kwanza ya kujua mwanamume anayekupenda ni pale anapokununulia gari."

Muhtasari

• Alisema kila mwanamume ana pesa lakini anachagua mwanamke wa kuzitumia kwake na kupuuzilia mbali dhana ya wanaume kusema kwamba hawana

Image: Hisani

Mrembo mmoja ambaye anajiita mshawishi na mtaalamu katika ushauri wa mambo ya mapenzi na ndoa mitandaoni amezua ghadhabu miongoni mwa wanaume baada ya kutoa ushauri unaoegemea upande mmoja akiwataka warembo kuwabwaga wanaume wasiowapa zawadi za magari.

Katika video hiyo ambayo imezua mjadala pevu, mrembo huyo aliwashauri warembo ambao wanaingia kwenye uchumba mpya kuwapa wachumba wao kipindi cha mwaka mmoja kupima upendo wao kwao.

Kwa mujibu wake, mwanamume ambaye anakupenda, haiwezi kupita mwaka mmoja kama hajakununulia zawadi ya gari, na kama mtaadhimisha mwaka mmoja katika uchumba pasi na yeye kukupa gari basi wewe mrembo jua hapo hakuna mapenzi na unafaa kujiita mkutano kujiuliza unachosubiri katika uhusiano wa aina hiyo.

“Warembo, kama umechumbiana na mwanamume kwa mwaka mmoja na bado hajakununulia gari moaka sasa, achana naye. Kwa nini nakushauri uachane naye? Mwanamume ambaye hajakununulia gari na umechumbiana naye kwa angalau mwaka mmoja, huyo hakuthamini.”

“Kwa sababu kama mwanamume anakuthamini, ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja atakununulia gari. Njia ya kwanza ya kujua mwanamume anayekupenda ni pale anapokununulia gari. Wanaume huwa hawanunulii gari wanawake ambao hawapendi.”

“Ishara ya kwanza ya mwanamume ambaye anakupenda, ni aina ya gari analokununulia. Kwa hivyo kama mpenzi wako wa kiume hajakununulia gari ni pengine wewe ndio mpango wa kando ama hakuthamini. Hivyo kama umekuwa hapo kwa mwaka na hajakununulia gari, rafiki yangu vunja huo uhusiano.”

Akiongea zaidi, mshawishi huyo aliwataka wanawake kuacha uhusiano huo na kumwacha tu mwanaume huyo.

Alisema kila mwanamume ana pesa lakini anachagua mwanamke wa kuzitumia kwake na kupuuzilia mbali dhana ya wanaume kusema kwamba hawana pesa pindi wapenzi wao wanapoomba kufanyiwa kitu Fulani.