"Hii imezidi sana!" Kabi amuonya Bahati kwa kumshika mkewe Milly kwa njia iliyomtia wasiwasi

Muhtasari

• Kabi alionekana akilalamika dhidi ya mwanamuziki Bahati kwa kucheza densi na mke wake Milly huku akiwa amemshika.

•Familia ya Wajesus na ile ya Bahati zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa muda mrefu.

Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Mwanamuziki na mjasiriamali maarufu alizindua kitabu chake cha kwanza 'Akothee Quotes' siku ya Jumamosi.

Akothee alizindua kitabu chake katika hoteli ya Eka, jijini Nairobi ambapo alikuwa amewaalika watu wengi mashuhuri wakiwemo wafanyibiashara, viongozi wa serikali na wasanii wenzake.

Wakati huo huo pia alizindua albamu mpya 'Sibuor Madhako' katika hafla hiyo ambayo mgeni mkuu alikuwa Wakili  PLO Lumumba.

The Wajesus Family, Bahati, Familia ya Kabu, Dr Ofweneke, Sandra Dacha na Dkt Ezekiel Mutua ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao walihudhuria hafla hiyo.

"Akothee tuko hapa kukusherehekea. Hongera ," Kabi alisema kupitia Instastori zake.

Katika chapisho lake lingine Kabi alionekana akilalamika dhidi ya mwanamuziki Bahati kwa kucheza densi na mke wake Milly huku akiwa amemshika.

Kabi ambaye ni wazi kuwa hakupendezwa na jambo hilo alimwagiza mgombea ubunge huyo wa Mathare kuondoka karibu na mkewe.

"Wewe wewe, toka hapo, unamshika sana wewe," Kabi alimwambia Bahati.

"Mtu amtag mke wake, hii imezidi," Aliongeza chini ya video ambayo alipakia.

Chini ya chapisho hilo Bahati alijitokeza kutetea tukio hilo huku akimuomba Kabi atulie.

"Apana sio poa manze," Kabi alimwambia Bahati.

Familia ya Wajesus na ile ya Bahati zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa muda mrefu. Mwaka jana hata hivyo kulikuwa kumetokea madai kuwa familia hizo hazipatani tena baada ya kutofautiana katika masuala ya kibinafsi.

The Wajesus na Bahati's hata hivyo walipuuzilia mbali madai hayo na hata kuonekana hadharani pamoja katika hafla tofauti.