"Nashukuru kuwa nawe maishani" Esther Musila aadhimisha miaka miwili tangu kukutana na Guardian Angel

Muhtasari

•Bi Musila ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 52 amesema kuwa hakuwahi fikiria urafiki wake na mwanamuziki huyo angekua kuwa ndoa.

•Wanandoa hao walifunga pingu za maisha mnamo Januari 4, 2022 katika harusi ndogo iliyohudhuriwa na familia na marafiki wa karibu.

Esther Musila ,52, na mumewe Guardian Angel ,32.
Esther Musila ,52, na mumewe Guardian Angel ,32.
Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

Wanandoa mashuhuri Peter Omwaka almaarufu Guardian Angel na Esther Musila wanaadhimisha miaka miwili tangu safari yao ya ndoa ilipong'oa nanga.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo Machi 13, 2020 na kadri siku zilivyosonga wakawa marafiki makubwa hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa mapema mwaka huu.

Akiadhimisha siku hiyo maalum maishanimwao, Bi Musila ameeleza kuwa alikuja kumtambua Guardian Angel kupitia wimbo wake 'Rada.'

Bi Musila ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 52 amesema kuwa hakuwahi fikiria urafiki wake na mwanamuziki huyo angekua kuwa ndoa.

"Hii ndiyo siku ambayo Bwana ameifanya. Tutafurahi na KUFURAHI ndani yake. Leo tunatimiza miaka 2 tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza, kwa hisani ya wimbo wa RADA. Muungano wetu usingetokea namna nyingine. Tulikuwa na mipango yetu lakini Mungu alitangulia mbele yetu na ameendelea kutuongoza katika safari yetu. Tazama Bwana amefanya yapi. Siku tulipokutana, sikuweza hata kufikiria jinsi urafiki wetu ungekuwa na maana kwangu na umbali ambao tumefikia. Ninashukuru kuwa na wewe katika maisha yangu. Furaha ya kumbukumbu ya urafiki mume wangu. Nakupenda," Musila alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Guardian Angel alienda chini ya ujumbe wa mkewe na kujibu "Nakupenda sana malkia wangu,"

Wanandoa hao walifunga pingu za maisha mnamo Januari 4, 2022 katika harusi ndogo iliyohudhuriwa na familia na marafiki wa karibu.