Samidoh azungumzia kushiriki mapenzi na wasichana wengi katika kijiji chao

Drama nyingi zimekumba ndoa ya Samidoh huku mkewe akizozana na mzazi mwenzake Karen Nyamu mara kadhaa.

Muhtasari

•"Samidoh huyu ni Eddy ametumia Pseudo. Umelima kijiji mzima mpaka ukapituka kwa jirani," shabiki alimwambia.

•Mwimbaji huyo alionekana kutupilia mbali tetesi hizo akijibu, "Bado" na kuambatanisha na emoji za kicheko.

Image: INSTAGRAM// SAMIDOH

Siku ya Alhamisi, msanii mashuhuri wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh alishiriki katika majibizano na mashabiki wake baada ya kuweka chapisho la kutatanisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Mwanamuziki huyo alichapisha meme ambapo mtumiaji wa Facebook alikuwa akijibu chapisho kuhusu ujumbe wake kwa mama mkwe.

"Asante kwa kunizalia tractor, imelima kijiji mzima," mwanamitandao huyo alikuwa amejibu katika meme hiyo.

Huku akizungumzia jibu la mwanamitandao huyo, Samidoh alisema, "Lakini hata kama ni kufunguka roho hamuoni kama mnaenda sana?"

Kama kawaida, mamia ya wanamitandao walimiminika katika chapisho la mwanamuziki wakiwa na maoni tofauti kwa meme hiyo.

"Samidoh huyu ni Eddy ametumia Pseudo. Umelima kijiji mzima mpaka ukapituka kwa jirani," Stellah Nyambura alimwambia.

Baba huyo wa watoto watano hata hivyo alionekana kutupilia mbali tetesi hizo akijibu, "Bado" na kuambatanisha na emoji za kicheko.

Njeri James alimuuliza, "Samidoh nilikuuliza tuko na masaa 24 kwa siku, unawezaje kushughulikia mabibi wawili na watoto tano, Unachunga raia,unaimba mugithii, Na Bado unapata time ya kucheat, wengine ata vyombo za last week hawajaosha."

Mashabiki wengine wengi pia walitoa maoni chini ya chapisho hilo huku wengi wakionekana kuzungumzia masaibu ya ndoa zao.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya staa huyo wa Mugithi kumsindikiza mkewe Edday Nderitu na watoto wao watatu hadi kwenye uwanja wa ndege wa JKIA ambapo waliabiri ndege kuelekea Marekani kwa likizo.

Siku ya Jumatatu,baba huyo wa watoto watano alichapisha picha yake, familia hiyo yake na bosi wa kampuni inayoaminika kufadhili safari hiyo wakiwa katika uwanja wa JKIA ila hakutoa maelezo kuhusu ziara hiyo.

"Safari ya Samburu," aliandika chini ya picha hiyo ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Drama nyingi zimekumba ndoa ya mwimbaji  huyo huku mkewe akizozana na mzazi mwenzake Karen Nyamu mara kadhaa.

Mapema mwaka huu, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi.

Hii ilikuwa baada ya mwanamuziki huyo kuonekana na Nyamu licha ya seneta huyo awali kudai uhusiano wao umefika mwisho.

Edday alimtaja Bi Nyamu kama mtu asiye na maadili na asiyeheshimu familia yake. Alidokeza kuwa takriban miaka mitatu iliyopita ya ndoa yake imejawa na maumivu na fedheha nyingi. Hata hivyo, alisema licha ya yote amebaki mwaminifu na ameendelea kuunga mkono kazi ya msanii huyo wa nyimbo za Kikuyu. 

"Umenifanya nionekane mjinga na kuchukulia ukimya wangu kuwa wa kawaida, nimekusaidia kuinua kipaji chako na kukuunga mkono kwa yote, lakini kitu kimoja nimekwambia na nasema hapa tena sitalea watoto wangu katika familia ya wake wengi," Edday alimwambia mwanamuziki huyo mwezi Februari.