Colonel Mustafa afunguka kuhusu video yake akifanya mjengo

Mustafa alikanusha kwamba video hiyo haikuwa ya wimbo mpya kama baadhi walivyosema bali ni ukweli ndio riziki yake anaipata mjengoni kutokana na ugumu wa maisha.

Muhtasari

• "Unapofanya kazi kuna maswala mengi, kunakuwa na beef pia na stori mingi kwa mjengo, kwa hiyo labda kuna mtu aliivujisha,".

Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Image: Colonel Mustafa (Instagram)

Rapa aliyegeuka mwigizaji Colonel Mustapha amevunja ukimya saa chache baada ya video yake akifanya kazi kwenye mjengo kuvuja mtandaoni.

Katika mahojiano maalum na Mpasho, Mustapha alithibitisha kuwa video hiyo ni ya kweli na alipatwa na wakati mgumu na kuamua kufanya kazi za ujenzi.

Rapa huyo aliambia Mpasho kuwa sio video ya muziki kama inavyodaiwa.

"Unapofanya kazi kuna maswala mengi, kunakuwa na beef pia na stori mingi kwa mjengo, kwa hiyo labda kuna mtu aliivujisha,".

Hi maze ni blunder, ni blunder," alieleza kuhusu aliyevujisha video hiyo.

"Baada ya habari hiyo kuvuja, nimeshindwa hata kutembea, kwani huwezi jitafutia, sasa itakuwa aje? Na siko vizuri hivo, mambo ni ngumu bana" alisema.

"Kuna kitu nilikuwa nakifanya siwezi kukizungumzia sana, lakini ni shughuli nimekuwa nikifanya kwa mwaka mmoja uliopita"

"Lakini sasa kuna msee tu hapo nadhani ni hivo kuna mtu alivujisha sikujua usiku ndio nilipata taarifa vile nimerudi"

Mustapha alielezea maisha yake kuwa magumu kwa muda. "Mambo yamekuwa magumu hapo nyumbani," alishiriki kwa ufupi.

Aliambia kwamba atazungumza zaidi juu ya safari yake ngumu baadaye.

Ameeleza hayo na rafiki yake "Unajua mafriends nimekuwa nawaambia, hawaskii" aliendelea kuongeza kuwa hakufanya tamasha lolote linalosababisha migogoro ya kifedha.

"Mara ya mwisho kutumbuiza ilikuwa nadhani mwaka jana Aprili hivyo kumekuwa mtu wangu," alikiri.

Alianza kazi za ujenzi ili kujiruzuku badala ya kuomba msaada wa umma.

"Hiyo kazi ni ngumu, inabidi saa zingine at least hata nimejaribu sana mwaka mmoja, kama ningeomba nimeomba kwa simu wangekuwa wame screenshot," alisema.

Mustapha pia alikiri kwamba mama yake ni mgonjwa na mahitaji yake ya matibabu ni ghali. Anafanyiwa chemotherapy.

"Hii kitu amekuwa nayo kwa muda wa miezi 8. Ni kichaa, mimi mwenyewe imekuwa noma,"