Nadia Mukami kusajili msanii mpya

Muhtasari

• Msanii wa kike Nadia Mukami amesema kwamba atakuwa anatambulisha kwa umma msanii wake wa kwanza chini ya lebo ya Sevens Creative hub, mnamo tarehe 1/02/2022.

• Kabla ya hapo atakuwa anafanya collabo na msanii huyo wiki kesho huku wengi wakisubiri kushuhudia kipaji hicho.

• Mpaka sasa haijafahamika iwapo chipukizi huyo atakuwa ni wa kiume ama wa kike, ikimaanisha kwamba italazimu mashabiki kusubiri hadi tarehe ya uzinduzi.

Nadia MUkami
Image: Hisani

Msanii wa kike Nadia Mukami amesema kwamba atakuwa anatambulisha kwa umma msanii wake wa kwanza chini ya lebo ya Sevens Creative hub, mnamo tarehe 1/02/2022.

Kabla ya hapo atakuwa anafanya collabo na msanii huyo wiki kesho huku wengi wakisubiri kushuhudia kipaji hicho.

Mpaka sasa haijafahamika iwapo chipukizi huyo atakuwa ni wa kiume ama wa kike, ikimaanisha kwamba italazimu mashabiki kusubiri hadi tarehe ya uzinduzi.

Swala kuu katika mchakato huu mzima, ni kupata maelezo kamili kuhusu urefu wa mkataba baina ya Sevens Creative hub na chipukizi huyo na mazingira ya kazi yatakuwa na sheria gani na pia msanii mwenyewe atakuwa na mikakati gani ya kustahimili uzito wa sanaa ya muziki hapa Kenya.

Lebo nyingi kwa kipindi Cha nyuma wamekuwa wakitofautiana na usimamizi wao kwa sababu ya hela, mashabiki wengi wakiamini kuwa mara hii hakutakuwa na mtafaruku huo ,ikifahamika kuwa Mukami alishawahi kupitia matatizo hayo na lebo tofauti na akajifunza kwayo.